HABARI MPYA

Your Ad Spot

Apr 27, 2017

KIONGOZI WA UPINZANI NCHINI ZAMBIA KUFUNGWA JELA AU KUNYONGWA

Mahakama nchini Zambia leo imekataa kufuta mashitaka ya uhaini dhidi ya kiongozi wa upinzani, Hakainde Hichilema, kesi ambayo imezusha wasiwasi wa kisiasa miezi kadhaa baada ya uchaguzi nchini humo uliobishaniwa.

Kiongozi huyo wa  chama cha United Party for National Development (UPND) alikamatwa  katika  msako  wa  polisi  nyumbani kwake mwezi  huu na  alifunguliwa  mashitaka  ya  kujaribu  kuipindua  serikali baada ya kufikishwa katika  mahakama  kuu. 

Mawakili  wa  Hichilema wamekata rufaa, wakisema  madai  hayo  hayaeleweki, lakini  jaji  Greenwell Malumani  aliiambia  Mahakama  iliyokuwa  imejaa  watu  kwamba  mahakama  hiyo  haina  mamlaka  ya kufuta madai  hayo na  kuipeleka  kesi  hiyo katika  mahakama  kuu.

Zambia  ilikuwa  moja  kati  ya  nchi  zenye utulivu  mkubwa  katika  eneo  la  kusini  mwa  Afrika  hadi  pale  mahusiano yalipoharibika  kati  ya  serikali  na  upinzani mwezi  Agosti, wakati  chama  cha  Rais  Edgar Lungu  cha  Patriotic  Front  kukishinda chama  cha  UPND katika  uchaguzi ulioelezwa kugubikwa  na  machafuko.
Source: Reuters/R. Ward

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages