LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Mar 31, 2017

WANACCM TISA WANADAIWA KUFA MJAWA KUTOKANA NA MATUKIO YANAYOENDELEA YA MAUAJI


Na Mwamvua Mwinyi, Pwani
VIONGOZI na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tisa kata ya Mjawa wilaya ya Kibiti, wanadaiwa kuawa kwa kupigwa risasi na wengine kuchomwa moto kutokana na matukio ya mauaji ya mfululizo yanayoendelea wilayani hapo .
Aidha CCM mkoa na Taifa imeombwa kutupia macho suala hilo kwa upana na kulisimamia ili kubaini chanzo halisi kinachosababisha wauawe.
Kutokana na hali hiyo wanachama wa maeneo ya wilaya hiyo, wanashindwa kuvaa sare za chama na kuogopa kuitana majina ya vyeo vyao.
Mwenyekiti wa CCM kata ya Mjawa ,Abubakar Seif, alisema baadhi ya viongozi wa vijiji na vitongoji wanashindwa kwenda ofisini kutekeleza majukumu yao.
Akizungumza katika mkutano wa ndani katika kata hiyo,ulioitishwa na chama hicho mkoa alisema wanaishi kwa sintofahamu na imani inawatoweka.
Abubakar alisema watu wanakiogopa chama kwasasa na kukimbia miji na ofisi zao.
Anaeleza miaka ya nyuma watu walikuwa wakigombea nafasi mbalimbali za uongozi lakini kwa sasa wanakwepa na kuhofia uhai wao.
Abubakar alikiomba chama kiendelee kwa nguvu zake kutoa hamasa kwa wanachama wa Rufiji na Kibiti kurejesha amani kwa vijana.
"Ni mashaka makubwa kwanini wauwe viongozi wa CCM pekee, sawa kila mtu na umauti wake lakini si kihivii "
"Tatizo hapa ni masuala ya kisiasa ambapo ukanda huu unatawaliwa na mvutano wa kisiasa toka huko nyuma "alisisitiza.
Katibu wa CCM Kibiti, Zena Mgaya, alisema ulinzi ni wa kila mmoja ili kusaidiana na jeshi la polisi.
Aliomba waendelee kukipenda chama na kukisimamia kwani vitendo hivyo vinadhibitiwa kwasasa.
Zena alieleza haiwezekani chama kikakaa bila viongozi wa chini, amewapa moyo wasikate tamaa hali itakayosababisha kuendelea kushika dola.
Alisema Polisi wametanda kila kona kwa sasa hivyo amani itarejea.
Zena alisema homa na mtikisiko uliopo kwenye wilaya ya Kibiti na Rufiji inaumiza jamii hasa wanaccm na viongozi wake ambao hawaishi kwa raha saa 12 jioni inabidi waingie ndani kujifungia.
Aliyekuwa katibu wa CCM mkoani Pwani anaesubiri makabidhiano, Hassan Mtenga, alitoa pole na kusema amepokea changamoto hiyo na ataikabidhi kwa katibu aliyeteuliwa sasa Anastasia Amas.
Ni matukio takriban 11 ya mauaji ya viongozi mbalimbali wa chama, wenyeviti wa vijiji na vitongoji ambayo yanadaiwa kujitokeza wilayani Rufiji na Kibiti.
Katika matukio hayo ni pamoja la March 28 ambapo mwenyekiti wa (CCM) tawi la  Mparange na mjumbe wa serikali ya kijiji cha Ikwiriri Kaskazini ,wilayani Rufiji mkoani Pwani, Michael Lukanda,aliuawa kwa kupigwa risasi ya kichwani na watu wasiojulikana.
Jingine ni march 12,mwenyekiti wa kitongoji cha Kazamoyo Hemed Njiwa aliuawa kwa kupigwa risasi.
Jan 19,mjumbe wa serikali ya kijiji cha Nyambunda ,Oswald Mrope, aliuawa kwa kupigwa risasi.
March 1,mwenyekiti wa kijiji cha Nyambunda Said Mbwana aliuawa.
Feb 24,watu watatu akiwemo afisa upelelezi wa polisi wilaya ya Kibiti Peter Kubezya aliuawa kwa risasi.
Octoba 24,2016 afisa mtendaji wa kijiji cha Nyambunda Ally Milandu alipigwa risasi na kufa na novemba 6,2016 ,mwenyekiti wa kitongoji cha Nyang'unda kijiji cha Nyambunda Mohammed Thabiti alipigwa risasi akielekea kwake.
Jeshi la polisi Pwani na serikali mkoani hapa, linaendelea kupambana kufuatia matukio hayo na kuimarisha ulinzi ikiwemo kusitisha usafiri wa bodaboda ifikapo saa 12 jioni

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages