Tuesday, March 21, 2017

'UVAMIZI' WA MAKONDA HAUNA MAJERUHI WALA PURUKUSHANI?

Na Charles Charles
 
Inawezekana kweli alikwenda. Lakini hii lugha ya kwamba eti "amevamia" ama "ameteka" ni kuongeza chumvi.

Hivi panapovamiwa au kutekwa kunakuwa hakuna purukushani, hakuna majeruhi hata mmoja wala patashika ya aina yoyote? 

Pili, kwa nini inasemwa kwamba alikwenda na askari/wanajeshi wenye silaha wakati picha ile anaonekana afisa usalama mmoja tu ndiye ana bunduki? 

Mbona yule askari polisi hana hata manati, lakini tunaambiwa "watu wenye silaha" utadhani zaidi ya mmoja? 

Tatu, mbona mara nyingi tunaona wakuu wa mikoa wanapokwenda "site" huwa wamezungukwa ama kulindwa na polisi, tena zaidi ya mmoja huku wamebeba bunduki na mchana kweupe? Nani kati yetu aliyewahi kulihoji hili?
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.