Dkt.SHEIN:NI MUHIMU NCHI WA WANACHAMA WA IORA KUIMARISHA USHIRIKIANO


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amesisitiza haja ya kuimarisha mashirikiano kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Nchi zinazopakana na Bahari ya Hindi (IORA), hatua ambayo itasaidia kwa kiasi kikubwa kukuza uchumi kwa nchi hizo sambamba na kuzitafutia ufumbuzi changamoto zilizopo.


Dk. Shein aliyasema hayo leo katika Mkutano wa kwanza wa wakuu wa nchi na Serikali wa Jumuiya ya nchi zinazopakana na Bahari ya Hindi (IORA), unaofanyika Mjini Jakarta Indonesia, mkutano ambao unaenda sambamba na maadhimisho ya miaka 20 ya Jumuiya hiyo.Pia Dk. Shein alisema kuwa umefika wakati kwa nchi hizo wanachama wa Jumuiya ya IORA kuimarisha zaidi ushirikiano pamoja na kutatua changamoto zilizopo zikiwemo hali ya usalama, kupambana na uharamia baharini , vita dhidi ya madawa ya kulevya, Ugaidi, athari za tabia nchi na mambo mengine yanayoweza kuleta athari katika nchi wanachama.Dk. Shein, alitoa wito kwa nchi hizo wanachama wa Jumuiya ya IORA kuongeza kasi katika utekelezaji wa malengo na maazimio ya Jumuiya hiyo ikiwa ni pamoja na kuitekeleza dhana ya uchumi wa habari iliyoanzishwa mwaka 2015 na Jumuiya hiyo.Kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Dk. Shein alisaini makubaliano yaliyofikiwa na Jumuiya hiyo katika Mkutano huo na kuahidi kwa Tanzania itachukua juhudi za makusudi katika kuyatekeleza makubaliano hayo kwa lengo la kuimarisha Jumuiya hiyo.

0 comments:

Post a Comment

Mdau, Uwanja huu ni wako, Toa maoni yako yasaidie kujua wewe unafikiri nini kifanyike kuboresha zaidi maisha ya Watanzania. Maoni yako yasilenge kuchochea mtafaruku katika jamii, kisiasa, kidini, kikabila au kijinsia. Mawasiliano yetu:- simu +255 (0) 712 498008, Email: nkoromo@gmail.com.
Bashir Nkoromo
Msimamizi Mkuu, Blog ya Taifa ya CCM.