CHARLES CHARLES: HIZI NDIZO KAZI NILIZOFANYA NILIPOKUWA SINGIDA - (SEHEMU YA KWANZA)

Aliyekuwa Katibu wa CCM wa Wilaya ya Singida Mjini, Ndugu Charles Charles (aliyesimama kushoto), akizungumza na wajasiriamali wa soko la mbogamboga (picha ya juu na chini) lililopo kata ya Mughanga linalomilikiwa na CCM wilaya hiyo.

Kikaokazi baina ya aliyekuwa Katibu wa CCM wa Wilaya ya Singida Mjini, Ndugu Charles Charles na Makatibu wa CCM wa Kata 18 za wilaya hiyo (picha ya juu na chini) alipowaita ofisini kwake ili kuwapa maelekezo yanayohusu majukumu yao.

Aliyekuwa Katibu wa CCM wa Wilaya ya Singida Mjini, Ndugu Charles Charles (picha ya juu, kati na chini) akikagua maduka ya wapangaji wa Chama hicho ili kuona ukubwa wa kila moja na kuangalia viwango vya kodi zinazolipwa na kulinganisha na bei ya soko ili kuona kama vinalingana.


Baadhi ya wajasiriamali wanawake wanaofanya biashara zao kwenye soko la mbogamboga katika eneo la Msufini, kata ya Mughanga wakimsikiliza aliyekuwa Katibu wa CCM wa Wilaya ya Singida Mjini, Ndugu Charles Charles (hayupo pichani) alipowaita ofisini kwake ili kusikiliza kero zao na kuzitolea majibu.
Aliyekuwa Katibu wa CCM wa Wilaya ya Singida Mjini, Ndugu Charles Charles (aliyeketi kwenye benchi) akisikiliza maelezo ya utangulizi kutoka kwa Kaimu Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) wa Wilaya hiyo, Ndugu Dhikiri Mohammed alipowatembelea akina mama lishe wanaofanya shughuli zao kwenye soko la mbogamboga linalomilikiwa na Chama hicho lililopo eneo la Msufini, kata ya Mughanga na kusikiliza kero zao kutoka banda moja hadi jingine.
Aliyekuwa Katibu wa CCM wa Wilaya ya Singida Mjini, Ndugu Charles Charles (aliyesimama  kulia huku akiwa amenyosha mkono wake), akizungumza na wajasiriamali wanaofanya shughuli zao kwenye soko la mbogamboga la Msufini, kata ya Mughanga ambalo linamilikiwa na Chama hicho alipowaita ofisini kwake ili kusikiliza kero zao na kuzitolea majibu (Picha zote na Katibu wa Umoja wa Wazazi wa Wilaya ya Singida Mjini, Peter Mwenda).

0 comments:

Post a Comment

Mdau, Uwanja huu ni wako, Toa maoni yako yasaidie kujua wewe unafikiri nini kifanyike kuboresha zaidi maisha ya Watanzania. Maoni yako yasilenge kuchochea mtafaruku katika jamii, kisiasa, kidini, kikabila au kijinsia. Mawasiliano yetu:- simu +255 (0) 712 498008, Email: nkoromo@gmail.com.
Bashir Nkoromo
Msimamizi Mkuu, Blog ya Taifa ya CCM.