BALOZI MERO AWASILISHA HATI ZA UTAMBULISHO


Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa, Mhe. Modest J. Mero akitoa maelezo mafupi kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mhe. António Guterres kabla ya kuwasilisha rasmi Hati za Utambulisho.
Balozi. Modest J. Mero akiwasilisha Hati za Utambulisho kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mhe. António Guterres.
Balozi. Modest J. Mero na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mhe. António Guterres wakipeana mikono baada ya zoezi la kuwasilisha Hati za Utambulisho kukamilika
Balozi. Modest J. Mero na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mhe. António Guterres wakisalimiana na maafisa wa Ubalozi wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa waliokuwepo kushuhudia tukio la kukabidhi Hati za Utambulisho (pichani wakisalimiana na Bw. Songelael Shilla, Afisa Mwandamizi wa Ubalozi wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa, New York).
Akizungumza baada ya makabidhiano ya Hati za Utambulisho, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bw. Guterres alisema Umoja wa Mataifa unaishukuru Tanzania kwa jinsi inavyojitolea kwa hali na mali katika jitihada za kumaliza migogoro ya kisiasa katika Ukanda wa Maziwa Makuu. 

Alitaja hatua zinazochukuliwa na Tanzania kurejesha amani DRC, Burundi na Sudan Kusini kuwa ni mfano wa kuigwa na kwamba anayo imani kwamba jitihada hizo hazitakoma mpaka nchi za SADC na EAC zote ziwe na utulivu wa kisiasa.Naye Balozi Mero akitoa neno la shukurani, alimuahidi Bw. Guterres ushirikiano wa karibu kati ya Tanzania na Umoja wa Mataifa katika kufanikisha malengo ya maendeleo na ulinzi wa amani. 

Aidha, alimwonyesha matarajio iliyonayo Tanzania kwake kwa kuzingatia ushirikiano mzuri aliounesha wakati alipokuwa akishughulikia masuala ya wakimbizi duniani, ambapo kwa pamoja na serikali ya Tanzania waliweza kutekeleza mengi kwa mafanikio makubwa

0 comments:

Post a Comment

Mdau, Uwanja huu ni wako, Toa maoni yako yasaidie kujua wewe unafikiri nini kifanyike kuboresha zaidi maisha ya Watanzania. Maoni yako yasilenge kuchochea mtafaruku katika jamii, kisiasa, kidini, kikabila au kijinsia. Mawasiliano yetu:- simu +255 (0) 712 498008, Email: nkoromo@gmail.com.
Bashir Nkoromo
Msimamizi Mkuu, Blog ya Taifa ya CCM.