LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 6, 2017

RAIS DKT. MAGUFULI AMUAPISHA MKUU WA MAJESHI YA ULINZI YA TANZANIA (CDF) PAMOJA NA VIONGOZI WENGINE IKULU JIJINI DAR ES SALAAM


Mkuu wa Majeshi, Jenerali Venence Salvatory Mabeyo, akila kiapo mbele ya Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Rais John Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam, Februari 6, 2017.
Mnadhimu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Luteni Jenerali, James Alois Mwakibolwa, akila kiapo mbele ya Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Rais John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam


Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimvisha cheo Luteni Jenerali Venance Mabeyo kuwa Jenerali kabla ya kumuapisha kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi kwenye Ukumbi wa mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Kamishna Jenerali Juma Malewa kuwa Kamishna Jenerali wa Magereza, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Luteni Jenerali Paul Meela kuwa Balozi nchini DRC Congo, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mkuu mpya wa Majeshi ya Ulinzi ya Tanzania Jenerali Venance Mabeyo mara baada ya tukio la uapisho lililofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Nyakimura Muhoji kuwa Katibu wa Tume ya Utumishi, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein (wakwanza kushoto), Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wapili kulia pamoja na Mkuu mpya wa Majeshi ya Ulinzi ya Tanzania Jenerali Venance Mabeyo mara baada ya uapisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein akizungumza mara baada ya tukio la Uapisho wa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Tanzania pamoja na  Viongozi mbalimbali Ikulu jijini Dar es Salaam.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein (watatu kushoto), Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wanne kutoka (kulia) , Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi (wakwanza kushoto), Mkuu mpya wa Majeshi ya Ulinzi ya Tanzania Jenerali Venance Mabeyo (watatu kutoka kulia ), Mnadhimu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Luteni Jenerali James Mwakibolwa (wapili kutoka kushoto),  Kamishna Jenerali wa Magereza Juma Malewa(wapili kutoka kulia) pamoja na Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Hamis Juma(wakwanza kulia) Ikulu jijini Dar es Salaam.



Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Mkuu wa Jeshi la Polisi  (IGP) Ernest Mangu mara baada ya tukio la Uapisho Ikulu jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages