LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 24, 2017

PROF.NDALICHAKO :SERIKALI INATARAJIA KUAJIRI WALIMU WA MASOMO YA SAYANSI ZAIDI YA 4,000

 Waziri wa Elimu,Sayansi,Teknolojia na Ufundi,Profesa Joyce Ndalichako akizungumza na wananchi wa Jimbo la Rifiji Mkoani Pwani.
 Mbunge wa Jimbo la Rufiji,Mohamed Mchengerwa (CCM)  akizungumza na wananchi wa eneo hilo.
Waziri wa Elimu,Sayansi,Teknolojia na Ufundi,Profesa Joyce Ndalichako akiwa na Mbunge wa Jimbo la Rufiji,Mohamed Mchengerwa (CCM) wakiongozama na wanafunzi wa sekondari ya Utete.
Waziri wa Elimu,Sayansi,Teknolojia na Ufundi,Profesa Joyce Ndalichako,amesema serikali inatarajia kuajiri walimu wa masomo ya sayansi zaidi ya 4000 ili kupunguza tatizo la uhaba wa walimu hao nchini.
Profesa Ndalichako aliyasema hayo juzi katika ziara yake Wilayani Rufiji ambapo ambapo alieleza kuwa kipaumbele kitatolewa katika shule za wilaya hizo ambazo kila aliyotembelea alikuta zina uhaba wa walimu hao na zingine hazina kabisa kwa miaka zaidi ya mitano.
Akiwa katika Shule ya Sekondari Utete ambapo aliongozana na Mbunge wa Jimbo la Rufiji,Mohamed Mchengerwa (CCM) alieleza kusikitishwa na kufeli kwa wanafunzi wengi katika mitihani ya kidato cha nne Mwaka jana na kuwaeleza kuwa serikali itajitahidi kutatua changamoto zilizopo ili wanafunzi wasipate kisingizio cha kufeli.
‘’Jitihada za Mbunge wenu anavyowaongelea ndani ya bunge zimenileta hapa leo kutokana na serikali hii kuwa sikiivu lakini nimesikitishwa na matokeo yenu ya Mwaka jana mmefeli sana lakini nimeona changamoto zilizopo katika shule yenu ikiwemo ukosefu wa walimu hasa wa sayansi,kutokuwepo kwa vifaa vya maabara tutawaletea mwezi huu na uchakavu wa vyoo tutajitahidi kurekebisha’’alisema Ndalichako
Aidha Ndalichako aliwaasa wanafunzi katika shule zote alizotembelea wilayani humo kuacha kuchanganya mambo na kuendekeza kwenye ngoma,muziki au kujihusisha na mahusiano ya kimapenzi kwani mambo hayo yanachangia kwa kiasi kikubwa wanafunzi kufeli.
Kwa upande wa Mchengerwa aliwataka wanafunzi kujibidiisha na masomo kwa kuwa katika kipindi cha uongozi wake anajitahidi kuishawishi serikali kuboresha elimu katika wilaya hiyo ili waweze kuzalisha wasomi wengi ambao kwa pamoja wataweza kuendeleza wilaya yao.
‘’Naombeni mshikilie elimu msome sana kwani nimejitahidi kuisukuma serikali na hatimaye  waziri amekuja kuona changamoto zetu na kuzitaftia ufumbuzi ,tusirudi nyuma tunatakiwa kuzalisha maprofesa wengi ambao tutashirikiana kuijenga Rufiji mpya’’alisema Mchengerwa
Hata hivyo Mchengerwa aliipongeza serikali kwa kusajili Shule ya Umwe ambayo wanafunzi walikuwa wanapata shida kusoma shule mbili tofauti kwa kuwa hawakuruhusiwa kufanya mitihani yao katika shule ambayo haijasaliwa na kwamba kilichobaki ni mkuboresha miundombinu ya shule hiyo.

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages