Wednesday, February 8, 2017

KINANA AONGOZA LEO MAZISHI YA MJUMBE WA NEC WILAYA YA MWANGA, ALIYEFARIKI KWA AJALI YA GARI AKITOKA KWENYE MAADHIMISHO YA MIAKA 4O YA CCM

 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana (wa sita kulia) akishiriki kuswalia  jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mjumbe wa NEC, Wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro, Mwalimu Ali Mbaga, wakati wa mazishi yaliyofanyika leo Feb 8, 2017, katika kijiji cha Kighare, Usangi wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro. Mbaga ni miongoni mwa viongozi wanne wa CCM, waliofariki kwa ajali ya gari wakati wakitoka kwenye maadhimisho ya miaka 40 ya CCM katika mkoa huo.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwasili kwenye Ofisi ya CCM mkoa wa Kilimanjaro, leo tayari kwenda kuongoza mazishi ya Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Ally Mussa Mbaga, katika kijiji cha Kighare, Wilayani Mwanga katika mkoa huo.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisaini kitabu cha wagenikatika Ofisi hiyo. Wapili ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kilimanjaro Iddi Juma na kulia ni Katibu wa CCM wa mkoa huo, Deogratius Ruta.
Katibu Mkuu wa CCM,Adulrahman Kinana akisalimina na Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Shaka Hamdu Shaka, alipowasili nyumbani kwa marehemu Mbaga, kuongozamazishi hayo. Katikati ni Katibu wa CCM mkoa waKilimanjaro Deogratius Ruta.
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akisalimia viongozi wa CCM alipowasili nyumbani kwa marehemu Mbaga, kuongozamazishi hayo
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akisalimia wananchi alipowasili nyumbani kwa marehemu Mbaga, kuongozamazishi hayo.
Nyumbani kwa marehemu Mbaga  yalikofanyikia mazishi hayo.
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akiongoza kwenda  nyumbani kwa marehemu Mbaga, kuongozamazishi hayo. Kulia ni Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akiongoza kwenda  nyumbani kwa marehemu Mbaga, kuongozamazishi hayo.
Katibu wa CCM wilaya ya Mwanga, Mwanaidi Mbisha (kushoto) akisimama kumkaribisha Katibu Mkuu, nyumbani kwa marehemu Mbaga.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimpa pole, Baba mdogo wa Marehemu Mbaga, Karim Mkando alipofika nyumbani kwa marehemu.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Said Mack Sadick akiwasili kwenye mazishi hayo.


Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akibadilishana mawazo na Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Said Meck Sadick kabla ya mazishi hayo. Kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Skaha Hamdu Shaka na Mkuu wa Wilaya ya Mwanga, Kipi Warioba.
Kinana akisalimia waombolezaji wakati akienda eneo maalum la shughuli za mazishi hayo.
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akifurahia jambo na Naibu Katibu Mkuu wa CWT, Oluochi kwenye eneo la shughuli za mazishi hayo.
Kinana akishauriana jambo na Said Meck Sadick, kwenye eneo la shughuli za mazishi hayo. Kushoto ni Shaka Hamdu Shaka.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Said Mecky Sadick akitoa rambirambi kwenye mazishi hayo.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akitoa salam rambirambi zake binafsi, za  CCM na za Mwenyekiti wa CCM Rais Dk. John Magufuli wakati wa mazishi hayo
Mwenyekiti wa CWT mkoa wa Kilimanjaro, Omar Mchome akitoa salamza rambirambi kwenye mazishi hayo. Marehemu Mbaga alikuwa Katibu wa CWT mkoa wa Kilimanjaro.
Naibu Katibu Mkuu wa CWT, Oluochi akitoa salama za rambi rambi kwenye mazishi hayo.
Baadhi ya waombolezaji kwenye msiba huo.
Baba mdogo wa marehemu Mbaga, Karim Mkando, akitoa maneno ya shukurani, wakati wa mazishi hayo.
Baadhi ya waombolezaji kwenye mzishi hayo
Waombolezaji wakitoa ndani jeneza lenye mwili wa marehemu Mbaga kwa ajili ya kuswaliwa na kuzikwa mwili huo wa marehemu.
Waombolezaji wakipeleka jeneza lenye mwili wa marehemu Mbaga kwenye eneo la kuswaliwa wakati wa mazishi hayo.
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana Watatu kulia walioko mstari wa mbele, akishiriki kuswalia mwili wa marehemu Mbaga, wakati wa mazishi hayo.
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana Watatu kulia walioko mstari wa mbele, akishiriki kuomba dua wakati wa kuswalia mwili wa marehemu Mbaga, wakati wa mazishi hayo.
waombolezaji wakifikisha eneo la kaburi jeneza lenye mwili wa marehemu mbaya tayari kwa maziko.
Mwili wa marehemu Mbaga ukishushwa kaburini
Waombolezaji wakizika.
waombolezaji baada ya kuzika. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.