CCM YAOMBOLEZA VIONGOZI NA WANACHAMA WA CCM WALIOFARIKI KWA AJALI MKOANI KILIMANJARO

SALAMU ZA POLE NA RAMBIRAMBI
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimepokea kwa majonzi na masikitiko makubwa taarifa za vifo vya watu saba wakiwemo viongozi na wanachama wanne wa CCM ambao ni Ndg Ally Mmbaga, mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa na mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Mkoa, Ndg Arnold Swai, Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana (UVCCM) Wilaya ya Hai, Ndg Anastazia Innocent Malamsha, Mwenyekiti wa UWT Tawi la Chuo Kikuu cha Ushirika (Moshi) na Ndg Edwin Msele, Katibu wa Hamasa wa Shirikisho la Vyuo Vikuu Mkoa wa Kilimanjaro vilivyosababishwa na ajali ya barabarani katika eneo la Mwika, Wilaya ya Moshi Vijijini, Mkoa wa Kilimanjaro siku ya Jumapili ya Februari 5,  2017.

Ajali hiyo ilitokea majira ya jioni ikihusisha gari ya mizigo aina ya Fuso na Toyota Hilux Surf iliyokuwa imewabeba Viongozi wa CCM waliokuwa wakitoka katika kutekeleza majukumu ya Chama ya Maadhimisho ya Miaka 40 ya Kuzaliwa kwa CCM yaliyofanyika kimkoa Wilayani Rombo na kusababisha vifo vyao.

Kutokana msiba huo, Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana amemtumia salamu za rambi rambi Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro, Ndugu Iddy Juma, familia, ndugu, jamaa, marafiki pamoja na wanachama wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro kufuatia vifo vya Viongozi wetu. 

Wana CCM nchi nzima, tunawaombea majeruhi kupona haraka, na tunamuomba Mwenyezi Mungu aziweke mahali pema roho za Marehemu.
Imetolewa na,

HUMPHREY POLEPOLE
KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA, ITIKADI NA UENEZI

06/02/2017

0 comments:

Post a Comment

Mdau, Uwanja huu ni wako, Toa maoni yako yasaidie kujua wewe unafikiri nini kifanyike kuboresha zaidi maisha ya Watanzania. Maoni yako yasilenge kuchochea mtafaruku katika jamii, kisiasa, kidini, kikabila au kijinsia. Mawasiliano yetu:- simu +255 (0) 712 498008, Email: nkoromo@gmail.com.
Bashir Nkoromo
Msimamizi Mkuu, Blog ya Taifa ya CCM.