Saturday, January 14, 2017

WANASIASA ACHENI MZAHA KUIOMBEA TANZANIA BAA LA NJAA

Hakuna ubishi kwamba baada ya Rais Dk John Magufuli kuonyesha kusimamia vema rasilimali za nchi na maadili ya utendaji kazi kwa watumishi na watendaji wa umma, sasa wapinzani wamebaki mikono mitupu wakikuna vichwa kutafuta ajenda za kusema ili kuhalalisha kwa wananchi uwepo wao.

Katika kujaribu kutafuta 'Kick' baadhi ya wanasiasa kutoka kambi hiyo ya upinzani, wamefikia hatua ya kuyachukua mambo ya hatari kwa taifa, na kujaribu kuyafanya ajenda za kutokea.

Moja ya jambo ambalo ni la hatari, ni kauli walizozitoa hivi karibuni Kiongozi wa ACT-wazalendo Zitto Kabwe na Tundu Lissu wa Chadema, kwamba Tanzania imo katika baa la njaa.

Kibaya zaidi wametoa kauli hizo huku wakijua wazi kwamba, Rais wa Jamhri ya Muungano wa Tanzania Dk John Magufuli amekwishaeleza kwamba japokuwa njaa inaweza kuwa ipo hapa na pale nchini, lakini haijafikia katika kiwango cha kuitangaza kuwa ni baa la kitaifa.

Kutokana na kutambua kwamba si vizuri nchi kuitabiria kupata majanga, kwa uchache tusome maelezo yafuatayo, kuona uhalisi wa viwango vya njaa kufikia hatua ya kuwa baa la kitaifa:-

Ufaransa katika miaka ya 1780 hadi 1789, wakati wa kipindi cha utawala wa Mfalme Louis XVI,  Ilikuwa mwenye pesa anaweza kwenda sokoni kununua chakula akakosa chakula na tatizo ilikuwa baa la njaa.

Jiji la Paris kipindi hicho lilikuwa na watu ambao wanakadiriwa zaidi ya 650,000, ila chakula kilichovunwa katika nchi nzima, hakikuweza kutosheleza hata nusu ya wakazi wa jiji hilo.

Kwa mujibu wa Shirika la Chakula Duniani- WFP,  Mwezi wa nne mwaka jana 2016 nchi ya Pakistan, kati ya watu 10, 6 hawana uwezo kabisa wa kupata chakula  na utapia mlo umetamalaki Pakistan, hii ni kwa sababu ya baa la njaa.

Kutokana na adhari za baa la njaa Ethiopia miaka ya 1984 na 1985 baa la njaa liliuwa watu zaidi ya milion moja.

Pia kutokana pia na baa hilo la njaa Somalia miaka ya 1991 na 1992 watu 300,000 walifariki kwa kukosa chakula.

Kiufupi baa la njaa ni moto wa kuotea mbali, si mchezo kama baadhi ya wanasiasa kama kina Zitto na Tundu wanavyohubiri kuwa kwa sasa Tanzania tunalo baa hili la njaa.

Kwa mujibu wa  Umoja wa Mataifa baa la njaa ni pale ambapo utapia mlo unapozidi kiwango cha asilimia 30, pale ambapo watu wawili kati ya 10,000 hufa kila siku kutokana na njaa, na pale ambapo kunatokea uhaba mkubwa wa chakula katika maeneo yenye idadi kubwa ya watu.

Mfano kulingana na vigezo hivyo vya Umoja wa Mataifa, jiji la Dar es salaam lenye makadirio ya watu zaidi ya milion 5, kuwe na uhaba mkubwa wa chakula kama mchele, unga, maharage na viazi hiyo ndio maana ya baa la njaa. TUSIOMBEE BAA LA NJAA TUSILONALO
*Imeandikwana Shabani Shabani na kuboreshwa na Msimamizi Mkuu wa Blog hii, Bashir Nkoromo
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.