Thursday, January 19, 2017

RAIS DK MAGUFULI AKUTANA NA WAZIRI WA DENMARK, MZEE MKAPA, LEO IKULU

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 19 Januari, 2017 amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Maendeleo wa Denmark Martin Bille Herman, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Mazungumzo hayo yamehudhuriwa na Balozi wa Denmark hapa nchini Mhe. Einar Hebogard, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango.

Martin Bille Herman amesema katika mazungumzo hayo wamejadili kuhusu uhusiano na ushirikiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Denmark na pia wamekubaliana kuuimarisha zaidi hususani katika masuala ya maendeleo ya kiuchumi.

Wakati huo huo, Rais Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa Ikulu Jijini Dar es Salaam. 

Mkapa amesema lengo la kukutana na Mhe. Rais Magufuli ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ni kumpa taarifa juu ya kazi anayoendelea kuifanya ya kuwa mwezeshaji wa mazungumzo ya mgogoro wa kisiasa nchini Burundi.
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.