LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jan 11, 2017

NAPE AMTEUA YUSUPH SINGO KUWA MKURUGENZI MPYA WA IDARA YA MAENDELEO YA MICHEZO

Dar es Salaam
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye amemteua   Yusuph Singo Omari kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo  kujaza nafasi iliyo achwa wazi na Leornad Thadeo aliyehamishiwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi. 

Uteuzi huo umefanyika kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma ya mwaka 2002 kifungu namba 6, kifungu (1)(b) kikisomwa pamoja na kifungu namba 8 cha sheria hiyo.

Kabla ya uteuzi huo Yusuph Singo Omari alikuwa Mkufunzi Mwandamizi katika Chuo Kikuu cha Ardhi katika masuala ya Michezo.

Nape Moses Nnauye  pia amemshukuru aliyekuwa akikaimu nafasi hiyo kwa muda wote Alex Nkenyenge ambaye alifanya kazi zake kwa uadilifu na kujituma kwa kusimamia majukumu yote ya Idara kwa ukamilifu.

Aidha ametoa mwito kwa wanamichezo na wananchi  kwa ujumla kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Bw Yusuph Singo Omari atakapokuwa anatekeleza majukumu yake.

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages