Friday, January 20, 2017

MWAKYEMBE: RAIS HAKUKIUKA KATIBA KATIKA UTEUZI WA WABUNGE ALIOFANYA

Dar es Salaam
Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe, amesema, Rais Dk. John Magufuli hakukiuka Katiba ya Tanzania kwa kuwateua wabunge wawili wanaume.

Mwakyembe amesema hayo leo, kutoa ufafanuzi, wakati akizungumza na Uhuru FM,  kuhusu baadhi ya watu wakiwemo wanasiasa kuzua mjadala hususan katika mitandao ya kijamii, kwamba Rais Dk. Magufuli amevunja Katiba kwa uteuzi alioufanya hivi karibuni wa kuwateua Profesa Palamagamba Kabudi na Abdallah Bulembo kuwa wabunge.

Waziri Mwakyembe ameshangazwa na baadhi ya watu kushutumu uteuzi huo, akisema Katiba ya nchi inampa Rais nafasi ya kuteua na kutengua nafasi ya mtu yoyote aliyemteua.

 Amesema ni vema watanzania wakamuacha Rais afanyekazi zake ikiwemo kufanya teuzi kwa kuwa yeye ndiye anaona mtu gani anafaa wapi na nani amteue kwa wakati gani.    

Mwakyembe alisema kutokana na Mamlaka aliyonayo kikatiba, Wakati amefanya uteuzi huo wa wabunge, jana jioni alimteua Dk. Abdallah Possi kuwa Balozi, ambaye Kituo chake cha kazi na tarehe ya kuapishwa vitatangazwa baadae.

Alisema kufuatia uteuzi huo Ubunge wa kuteuliwa wa Dk. Possi ambaye alikuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, aliyekuwa akishughulikia Ulemavu, nao unakoma.
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.