Tuesday, January 10, 2017

MPOGOLO AONGOZA LEO MAZISHI YA ALIYEKUWAA KATIBU WA CCM WILAYA YA KILINDI

Na Bashir Nkoromo
Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo, ameongoza umati wanachama wa CCM na nawananchi kwa jumla, katika mazishi ya aliyekuwa Katibu wa CCM wilaya ya Kilindi mkoani Tanga, Hawa Nangaju, yaliyofanyika leo Januari 10, 2017, Mbagala, Dar es Salaam.

Katika mazishi hayo, walihudhuria pia viongozi kadhaa akiwemo Katibu wa Halmashauri Kuu Taifa(NEC) ya CCM, Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Kanali Mstaafu Ngemela Lubinza na Waziri wa Afya, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu na baadhi ya viongozi kutoka Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba.

Akizungumza kwenye mazishi hayo, Mpogolo alisema, Chama Cha Mapinduzi kimeondokewa na kiongozi ambaye alikuwa mwadilifu, mchapakazi na anayekipenda kwa dhati Chama, hivyo kimebakiwa na majozi makubwa kutokana na kifo cha katibu wake huyo.

"Ni kutokana na Chama kilivyomfahamu na kumwamini Hawa Omari Nangajau, ndiyo sababu sisi viongozi tuliobaki pamoja na wanachama wenzetu wa CCM, tumepokea msiba huu kwa majonzi makubwa, hivyo ili kumuenzi ni sisi kufanyakazi kwa uadilifu, kujituma na kukipenda Chama kama alivyokuwa akifanya", alisema Mpogolo.

Akisoma, wasifu, Mkuu wa Utawala Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Bakari Khamis Hamadi alisema, Marehemu Hawa Nanganjau aliyezaliwa Novemba 27, 1962 katika Kijiji cha Mkaramo Wilayani Kilwa mkoani Lindi alihitimu elimu yake ya sekondari katika shule ya Sekondari  Kibasila, Temeke, Dar es Salaam mwaka 2004.

Khamis alisema, amekuwa akifanya kazi mbalimbali katika CCM tangu mwaka 1981 akiwa katibu wa Tawi na kupita katika nafasi mbalimbali za ukatibu hadi nanafasi yake ya mwisho ya Ukatibu wa CCM wilaya ya Kilindi mkoani Tanga, tangu mwaka 2013 hadi mauti yalipomfika, Januari 8, 2017, kutokana na maradhi ya tumbo.
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rodrick Mpogolo (wapili kushoto), akiwa msibani wakati wa mazishi ya aliyekuwa Katibu wa CCM wilaya ya Kilindi Hawa Omari Nanganjau, yaliyofanyika leo nyumbani kwa marehemu, Mbagala, Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Ngemela Lubinza
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rodrick Mpogolo akisalimiana na Waziri wa Afya, Jinsia, Wazee na WatotoUmmy Mwalimu, wakati wa mazishi ya aliyekuwa Katibu wa CCM wilaya ya Kilindi Hawa Omari Nanganjau, yaliyofanyika leonyumbani kwa marehemu, Mbagala, Dar es Salaam. 
Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo na Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Kanali Mstaafu Ngemela Lubinza wakiwapa pole waombolezaji, wakati wa mazishi ya aliyekuwa Katibu wa CCM wilaya ya Kilindi Hawa Omari Nanganjau, yaliyofanyika leo nyumbani kwa marehemu, Mbagala, Dar es Salaam.
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.