Saturday, January 14, 2017

MKAPA AWATAKA WATANZANIA KULINDA NA KUTUNZA MBUGA ZA WANYAMA

Na Daudi Manongi-MAELEZO
Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Benjamini Mkapa amewataka watanzania kulinda na kutunza mbuga za wanyama kuwa ni urithi wa kila Mtanzania na kuzitaka nchi mbalimbali kusaidia katika kulinda urithi huo.

Pia mevitaka vyombo vya habari kushiriki vyema katika kutangaza mbuga za wanyama na kutangaza jitihada zinazofanywa na serikali katika kutokomeza ujangili wa aina mbali mbali ikiwemo wa pembe za ndovu.

 Mkapa metoa mwito huo wakati akizungumza baada ya kupokea matembezi ya kilometa tano yaliyoanzia Ubalozi wa China hadi Hoteli ya Sea Cliff  kwa lengo la kupigavita ujangili unaofanywa dhidi ya Tembo

Naye Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gen Gaudence Milanzi amewaasa wafugaji kuacha kuingiza mifugo katika hifadhi za taifa ili kuzitunza hifadhi hizo.

“Hifadhi za taifa hapa nchini hazina budi kulindwa na kutunzwa ili vizazi vijavyo viweze kuzifaidi kwani maeneo hayo yametengwa kwa ajili ya wanyama pori pekee na siyo kwa mifugo na hivyo kila mwananchi analo jukumu la kuyalinda mazingira haya,”Aliongeza Mej.Jenerali Milanzi.

Awali akizungumza katibu mkuu huyo alisema kuwa Serikali ina mkakati mkubwa wa kuhakikisha inashirikiana na nchi zingine katika kutokomeza kabisa Ujangili wa pembe za ndovu nchini.

Aidha aliishukuru Serikali ya Jamhuri ya watu wa China kwa kuwa mstari wa mbele katika kupambana na ujangili wa pembe za ndovu ikiwemo upigaji  marufuku biashara ya pembe za ndovu na viwanda vya kuchonga pembe hizo ifikapo mwezi machi Mwaka huu.

Mbali na hayo katibu Mkuu uyo amewaasa watanzania kuwafichua wale wote wanaojihusisha na biashara hiyo na kuonya kuwa kwa kushiriki katika biashara hii tutawafanya tembo wetu kuwa historia kwani hawatakuwepo tena.

Katibu Mkuu wa Asasi ya Tanzania – China Promotion Association (TCFPA), akitoa maelekezo kuhusu matembezi ya  Walk for Elephant Dar es Salaam 2017 mwishoni mwa matembezi hayo yaliyoishia kwenye viwanja vya hoteli ya Sea Cliff, Dar es Salaam, leo.
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.