Tuesday, January 31, 2017

KAULI YA SERIKALI BUNGENI KUHUSU MWENENDO WA HALI YA UCHUMI WA TAIFA

KAULI YA SERIKALI BUNGENI KUHUSU MWENENDO
WA HALI YA UCHUMI  WA TAIFAUTANGULIZI  1. Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Kanuni ya Bunge Na. 49 (1 ) ya Kanuni za Bunge toleo la Januari mwaka 2016, naomba kuwasiisha taarifa kuhusu hali ya uchumi  wa Taifa, hususan mwenendo wa viashiria mbalimbali vya uchumi, ikiwemo ukuaji wa uchumi, mfumuko wa bei, mwenendo wa sekta ya nje na akiba ya fedha za kigeni, mwenendo wa sekta ya fedha ikiwa pamoja na hali ya ukwasi na deni la Taifa.

  2. Mheshimiwa Spika, Serikali inatoa taarifa hii ili kukitaarifu chombo hiki muhimu cha wawakilishi wa wananchi kuhusu afya ya uchumi wa Taifa letu ili Waheshimiwa Wabunge waweze kuwafikishia wananchi ujumbe/maelezo sahihi badala ya uvumi wa mitaani.
             
    Ukuaji wa Pato la Taifa

  3. Mheshimiwa Spika, ukuaji wa uchumi ni mojawapo ya viashiria vinavyotazamwa katika kutathmini afya ya uchumi wa Taifa. Ukuaji wa uchumi unapimwa kwa kutumia ukuaji wa Pato la Taifa yaani thamani ya bidhaa na huduma zilizozalishwa katika nchi katika kipindi kinachorejewa ikilinganishwa na kipindi kilichopita. Takwimu za ukuaji wa Pato la Taifa zinaonesha kuwa uchumi wa Taifa umeendelea kukua na Tanzania imebaki kuwa miongoni mwa nchi za bara la Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara ambazo uchumi wake unakua kwa kasi kubwa zaidi. Naomba niwape mifano ya nchi jirani kama ifuatavyo.

    Jedwali1: Ukuaji wa Pato la Taifa Katika Baadhi ya Nchi za Kiafrika


NCHI

2015

2016 (Matarajio)

Burundi

-4.0

-0.5

Kenya

5.6

6.0

Rwanda

6.9

6.0

Tanzania

7.0

7.2

Uganda

4.8

4.9

Zambia

3.0

3.0

Malawi

2.9

2.7

Congo DRC

6.9

3.9

Afrika Kusini mwa Sahara

3.4

1.4  1. Mheshimiwa Spikakatika kipindi cha Januari hadi Septemba, 2016 kiwango halisi cha ukuaji wa Pato la Taifa kiliongezeka na kufikia wastani wa asilimia 6.5 ikilinganishwa na kiwango cha ukuaji cha asilimia 6.3 katika kipindi kama hicho mwaka 2015. Kwa ujumla....Inaendelea/>BOFYA HAPA
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.