Thursday, January 19, 2017

FES YA UJERUMANI YAMFAGILIA RAIS DK. MAGUFULI KWA MIKAKATI YA KUINOA UPYA CCM

NA BASHIR NKOROMO
Asasi ya Fredrich Ebert Stiftung (FES) ya Ujerumani, imeelezea kuvitiwa kwake na hatua anazofanya Rais Dk. John Magufuli, kukifanya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa kipya zaidi.

Taasisi hiyo imesema, inavutiwa na hatua hizo zinazofanywa na Rais Dk. Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi, kwa kuwa sasa zitakifanya kuwa cha watu zaidi badala ya kuwa mali ya viongozi kama kilivyokuwa kimeanza kuonekana.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi hiyo ya EFS hapa nchini, Michael  Schultheiss, alipokutana na kuwa na mazungumzo na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, anayeshughulikia Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI), Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo.

Amesema, hatua hiyo ya Rais Dk. Magufuli, itakiimarisha zaidi Chama Cha Mapinduzi, na kuendelea kuaminiwa na Watanzania wengi hivyo kukipa ridhaa ya kuunda serikali kwa kuwa na matarajio kuwa serikali inayoundwa na CCM itaweka mikakati iliyo bora katika kuwainua kiuchumi katika nyanja mbalimbali na kuifanya nchi kuwa yenye uchumi unaokua haraka.

Naye kanali Mstaafu, Lubinga alisema, CCM inaipongeza FES kwa kuendelea kuwa karibu na vyama vyote vya siasa hapa nchini, kwa kuwa hatua hiyo inavisaidia hasa vyama vichanga kuimarika katika misingi ya kujielewa kuwa vinayo majukumu ya kuwafanyia wananchi katika kusaidia kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika nchi.

Ameisihi FES kuendelea na jitihada zake hizo, hasa kwa Chama Cha Mapinduzi kwa kuwa kufanya hivyo ni moja ya njia zinazoimarisha uhusiano wa miaka mingi ulipo baina ya Chama na Taisisi hiyo.
 Katibu Msaidizi Mkuu Idara ya Siasa na Ushirikiano wa Kimataifa, Mama Juliana Chitinka akitoa maneno ya Utangulizi, kabla ya mazungumzo kuanza kati ya Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga na Mkurugenzi Mkazi wa FES, Michael Schulttheiss, leo katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam.
 Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga na Mkurugenzi Mkazi wa FES, Michael Schulttheiss, wakiwa tayari kwa mazungumzo leo katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mratibu wa Taasisi FES,  Amon Petro.
Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga (kulia) akisisitiza jambo wakati akizungumza na Mkurugenzi Mkazi wa FES, Michael Schulttheiss, leo katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam. Picha:Bashir Nkoromo)
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.