LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Dec 3, 2016

SHIRIKISHO VYUO VYA ELIMU YA JUU LA MTETEA RAIS DK MAGUFULI, KERO KUHUSU UTOAJI MIKOPO KWA WANAFUNIZI WA VYUO VIKUU

➤Lasema Rais ameshatimiza wajibu wake kwa kutoa fedha za mikopo

➤Ltaka lawama ziwashukie watendaji Bodi ya Mikopo
➤Wanafunzi hewa lawatupia lawama Bodi ya Mikopo
Na Bashir Nkoromo
Wadau wa elimu wametakiwa kutomlaumu Rais Dk. John Magufuli kuhusu kero zinazohusiana na mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu kwa kuwa ameshatekeleza wajibu wake kwa kutoa fedha, zinazokadiriwa kuwa Sh. bilioni 483 mwaka huu ambapo ni ongezeko la kadirio la sh. Bilioni 130, kutoaka kadirio la sh. Bilioni 350 la mwaka jana.

Hayo yamesemwa na Kaimu Katibu Mtendaji wa Shirikisho la Vyuo vya Elimu ya Juu-CCM, Katibu Msaidizi wa CCM, Daniel Zenda wakati akifungua mkutano mkuu wa uchaguzi wa Shirikisho hilo, tawi la Chuo Kikuu cha Dar es Salam, uliofanyika leo katika ukumbi wa DDC, Mwenge na kuongeza kuwa wanapaswa kulaumiwa ni watendaji wa serikali waliopewa jukumu la kuratibu na kutoa mikopo hiyo.

Zenda amesema, Rais Dk. John Magufuli, amekuwa akionyesha kiu ya kuhakikisha hali ya huduma katika sekta ya elimu kwenye vyuo vikuu inakuwa bora ikiwemo kuhakikisha kila mwanafunzi anayestahili kupata mikopo anapata bila vikwazo, lakini watendaji wamekuwa wanaonekana kutoishauri serikali vizuri na hivyo kusababisha kujitokeza kwa utata na vikwazo vya mara kwa mara hasa katika utoaji mikopo.

"Mimi ninavyoona kuna baadhi ya watumishi serikalini hasa pale Bodi ya mikopo ambao wangpenda Serikali ya Rais Dk. John Magufuli isifanikiwe katika azma yake ya kutaka kuboresha sekta mbalimbali ikiwemo elimu, kwa mfano inakuwaje watu waliopewa dhama ya kushauri wanaweka kipengele kama cha mlemavu asipewe mkopo hata akipata alama nzuri kwenye masomo yasiyo ya kipaumbele vya mikopo na wakati huo huo, kushauri kwamba ulemavu ni kipaumbele ni sifa mojawapo ya mwanafunzi kupata mikopo?", Zenda alihoji na kuongeza;

"Yaani hawa washauri wamekuwa wakielekeza mambo ya ajabu sana, sasa tazama hivi sasa wamekuja na sheria kwamba mwanafunzi atakayekuwa na umri wa miaka kuanzia 30 asipewe mkopo, wakati kila mmoja anajua wapo Watanzania wanaoweza kuchaguliwa kusoma vyuo vikuu wakiwa na umri huo, kwa kuwa katika kuchaguliwa kwenda vyuo vikuu hakuna kigezo cha umri".

Zenda aliwatupia lawama Bodi ya Mikopo akisema, kwamba migogoro mingi kuhusu mikopo huanzia kwao akitoa mfano kwamba, hata suala la kuwepo wanafunzi hewa kunatokana na ujanjaujanja wa watumishi katika bodi hiyo ili waweze kujipatia fedha za bure.

Aliwataka wanafunzi wa vyuo vikuu kuachana na tabia ya kudhani maandamano ni suluhisho la kuweza kupata mikopo wanapoikosa, na badala yake, inapotokea watumie Shirikisho hilo, kufikisha hoja zao kwa viongozi hadi ngazi ya taifa ambako bila shaka ufumbuzi hatimaye utapatikana.

"Sasa wewe unashawishiwa kuandamana, unakubali, haya ukishaandamana ndiyo unapata mkopo. acheni kabisa ujinga huu, ninyi ni wasomi mnachotakiwa ni kujenga hoja na kuzifikisha kunakohitajika", alisema Zenda.

Kuhusu uchaguzi huo aliwataka wajumbe kuchagua viongozi kwa kufuata sifa za kuwa wapambanaji kwa hoja, ni si kuchagua viongozi kwa kufuata urafiki au kupewa rushwa.
Kaimu Katibu Mtendaji wa Shirikisho la Vyuo vya Elimu ya Juu-CCM, Katibu Msaidizi wa CCM, Daniel Zenda wakati akifungua mkutano mkuu wa uchaguzi wa Shirikisho hilo, tawi la Chuo Kikuu cha Dar es Salam, uliofanyika leo katika ukumbi wa DDC, Mwenge Dar es Salaam. Picha na Bashir Nkoromo wa theNkoromo Blog. /Picha zaidi/>>BOFYA HAPA

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages