UCHAGUZI WA VIONGOZI WAPTA WA BARAZA LAVYAMA VYA SIASA KUFANYIKA DESEMBA 19, 2016

DAR ES SALAAM
Uchaguzi wa viongozi wapya katika Nafasi ya Mweneyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa nchini, utafanyika Desema 19, 2016, tarehe ambayo viongozi walipo sasa watakuwa watamaliza muda wao.

"Baraza la Vyama vya Siasa imewatangazia wajumbe wa Baraza la Vyama vya Siasa kuwa, kutakuwa na uchaguzi wa viongozi wa Baraza la Vyama vya Siasa utakaofanyika tarehe 19 Disemba, 2016 Dar-es salaam. Uchaguzi wa viongozi wa Baraza unafanyika kwa mujibu wa Kanuni za Baraza la Vyama vya Siasa." Imesema sehemu ya Taarifa iliyosambazwa na Katibu wa Baraza hilo la vyama vya siasa.
  
Taarifa imesema fomu za kugombea katika uchaguzi huo, zimeanza kutolewa leo saa tatu na nusu asubuhi, katika Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa jijini Dar es salaam na zinatakiwa kurejeshwa siyo zaidi ya tarehe 12 Disemba, 2016 saa tisa na nusu mchana katika Ofisi hiyo ya Msajili wa Vyama vya Siasa.

Kulingana na taarifa hiyo wasiweza kufika Ofisi ya Msajili wa vyama wanawezapia kupata fomu kutoka kwenye tovuti ya ofisi ya msajili www.orpp.go.tz ambako pia zinapatikana.

Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa imewaomba wajumbe wa Baraza la Vyama vya Siasa wenye nia ya kugombea nafasi hizo, kuchukua fomu, kuzijaza kikamilifu na kuzirudisha kwa wakati huku wakizingatia kwamba kanuni za Baraza la Vyama vya Siasa zinakataza mjumbe wa Baraza kugombea nafasi zaidi ya moja.

0 comments:

Post a Comment

Mdau, Uwanja huu ni wako, Toa maoni yako yasaidie kujua wewe unafikiri nini kifanyike kuboresha zaidi maisha ya Watanzania. Maoni yako yasilenge kuchochea mtafaruku katika jamii, kisiasa, kidini, kikabila au kijinsia. Mawasiliano yetu:- simu +255 (0) 712 498008, Email: nkoromo@gmail.com.
Bashir Nkoromo
Msimamizi Mkuu, Blog ya Taifa ya CCM.