LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Dec 6, 2016

SERIKALI KUANZA UTOAJI TUZO ZA UMAHIRI KWA WAANDISHI WA HABARI WA BLOG NCHINI MWAKANI

Na Beatrice Lyimo, DAR
SERIKALI imesema mwakani itaanza utoaji tuzo za umahiri kwa waandishi wa habari wa mitandao ya kijamii hususan wa Blog.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar  es salaam na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye wakati akifunga Mkutano Mkuu wa Tanzania Bloggers Network (TBN) na semina ya wanachama wa umoja wa waendeshaji wa blog nchini.

Waziri Nape alisema kuwa lengo la tuzo hizo ni kuzisaidia blogs za Tanzania kubobea katika nyanja tofauti ikiwemo kilimo, mifugo, viwanda, hifadhi ya jamii kwa nia ya kuipa heshima tasnia ya habari nchini.

Nape amesema tayari Serikali imeanza mazungumzo na  kampuni na taasisi mbalimbali kwa ajili ya kudhamini tuzo hizo ili kuhakikisha kuwa washindi wanapatikana kwa uwazi.

“Tuzo hizo zitakuwa za kwanza kwa namna zitakazovyoendeshwa kwa uwazi hivyo kampuni zaidi zinakaribishwa kuweza kuzidhamini mashindano hayo yatakayojielekeza kwenye nyanja tofauti” alisema Waziri Nape.

Waziri Nape amewataka wamiliki na watendaji wa blogs nchini kushirikiana na Serikali ili kuweza kuijenga nchi.

“Tutumie fursa za kisiasa zilizopo, fursa za teknolojia ili kuhakikisha tunajenga Tanzania tunayoitaka, ishaurini Serikali kwa kutumia taaluma mliyonayo ili kuweza kuipeleka nchi ya Tanzania tunayoitaka” alifafanua Waziri Nape

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages