BREAKING NEWS

Post Top Ad

Your Ad Spot

Wednesday, December 14, 2016

NAIBU KATIBU MKUU MPYA WA CCM-BARA, AWATAKA USHIRIKIANO WATUMISHI WA CCM KUTATUA CHANGAMOTO

Na Bashir Nkoromo
Naibu Katibu Mkuu mpya wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo, amesema, anazitambua changamoto zinazowakabili wafanyakazi wa Chama Cha Mapinduzi na kuahidi kushirikiana na wafanyakazi hao kuzipatia ufumbuzi.

Mpogolo amekutana na wafanyakazi hao ikiwa ni mara yake ya kwanza tangu alipoteuliwa kushika wadhifa huo, katika kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM, kilichofanyika jana, Ikulu jijini Dar es Salaam.

"Mimi nimekuwa katika chama hiki mda mrefu sana, kwa hiyo sehemu kubwa ya changamoto zinazowakabili wafanyakazi nazijua hivyo nitatumia juhudi zangu na maarifa kuhakikisha changamoto hizo zinapungua au kuisha kabisa".

"Lakini kubwa zaidi ni mimi na ninyi wafanyakazi kushirikiana kwa pamoja katika kupambana na changamoto hizi na hatimaye tukifikishe chama kunakotarajiwa, na bila shaka mnajua lengo kuu la Chama chochote ni kuwa na nguvu na inayokipa uwezo wa kuongoza kwa kushika dola", alisema Mpogolo.

Alisema, pamoja na kuwa katika Chama kwa mda wa kutosha kujifunza ana kuelewa mengi, lakini bado atahitaji ushauri kwa baadhi ya wafanyakazi wazoevu, hivyo wafanyakazi wasisite kumpa ushauri wao pale watakapokuwa wanaona kwamba ushauri wao utasaidia kusonga mbele.

Mpogolo aliwataka wafanyakazi kuongeza bidii ya kazi kila mmoja katika nafasi yake, akisema ni lazima watambue kuwa kila mfanyakazi wa Chama katika eneo aliloko mchango wake unahitajika sana, na aelewe kuwa isingekuwepo haya ya chama kumwajiri kama hakitarajii tija kutoka kwake.

Mapema, Mpogolo aliwasili ukumbini akifuatana na Naibu Katibu Mkuu mstaafu wa CCM, Rajab Luhwavi ambaye ameteuliwa hivi karibuni kuwa Balozi.

Luhwavi aliwaomba wafanyakazi kumpa ushirikiano Naibu Katibu Mkuu huyo mpya akimwelezea kuwa ni Kada wa Chama ambaye amefanya kazi katika idara nyingi na nyeti hivyo anayo hazina ya mambo mengi anayofahamu katika chama.
 Naibu Katibu Mkuu mpya wa CCM, Rodrick Mpogolo akiingia ukumbini kuzungumza na wafanyakazi wa Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba Dar es Salaam, leo. Kulia ni Mkuu wa Utawala bakari Hamad na wapili ni Katibu Msaidizi Mkuu Idara ya Utawala na Uendeshaji, Salum Khatib Reja.
 Naibu Katibu Mkuu mpya wa CCM, Rodrick Mpogolo akiwana na Naibu Katibu Mkuu mstaafu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi, alipowasili kuzungumza na wafanyakazi wa Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba Dar es Salaam, leo.
 Wafanyakazi wakishangilia ukumbini Mpogolo na Luhwavi walipowasili ukumbini
 Katibu Msaidizi Mkuu Idara ya Utawala na Uendeshaji,  Makao Makuu ya CCM, Salum Khatib Reja, akitoa utangulizi, baada ya Naibu Katibu Mkuu mpya wa CCM, Rodrick Mpogolo kuwasili ukumbini kuzungumza na wafanyakazi wa Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam, leo
 Wafanyakazi wakiwa tayari kumsikiliza Mpogolo
 Mkuu wa Utawala Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam, Bakar Hamad (kulia) akishirikiana na viongozi wenzake kunukuu dondoo, Naibu Katibu Mkuu pya wa CCM-Bara Rodrick Mpogolo alipozungumza na wafanyakazi wa Ofisi hiyo, leo Desemba 14, 2016. Kushoto ni Mwangalizi wa Ofisi Rose Francis na Ofisa Mwendeshaji Mwajuma Nyamka.
 Wafanyakazi wakiwa ukumbini
 Wafanyakazi wakiwa ukumbini
 Wafanyakazi wakiwa ukumbini 
 Naibu Katibu Mkuu mstaafu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi akimkaribisha Naibu Katibu Mkuu mpya wa CCM, Rodgrick Mpogolo (katikati), kuzungumza na wafanyakazi wa Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba Dar es Salaam, leo, Desemba 14, 2016. Kulia ni Katibu Msaidizi Mkuu Idara ya Utawala na Utumishi Makao Makuu ya CCM, Salum Khatib Reja.
  Naibu Katibu Mkuu mpya wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo akizungumza na wafanyakazi wa Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo Desemba 14, 2016. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM-Bara, Rajab
Naibu Katibu Mkuu mpya wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo akizungumza na wafanyakazi wa Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo, Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi na kulia ni Katibu Msaidizi Mkuu Idara ya Utawala na Uendeshaji, Salum Khatib Reja. PICHA BASHIR NKOROMO

No comments:

Post a Comment

Mdau, andikamaoni yako hapa yasaidie kujua wewe unafikiri nini kuhusu posti hii. Tafdhali, Maoni yako yasiwe ya uchochezi wa aina yoyote.. Mawasiliano yetu:- simu +255 (0) 712 498008, Email: nkoromo@gmail.com.
Bashir Nkoromo
Msimamizi Mkuu, Blog ya Taifa ya CCM.

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages