MWILI WA BRIGEDIA JENERALI MHAIKI WAAGWA RASMI LEO

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein ​akitia saini kitabu cha maombolezo ya kifo cha Kamanda wa Brigedia ya Kikosi cha Nyuki, Zanzibar, Brigedia Jenerali Cyril Ivor Mhaiki,  aliyefariki juzi katika  hospitali  ya Jeshi la Wananchi JWTZ Lugalo JIjini Dar es Salaam, baada ya kuugua kwa muda mfupi na kuagwa leo mjini Zanzibar.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiwa na ​W​aziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt.​​Hussein Ali Mwinyi  (kushoto) na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Davis Mwamunyange 
 Baadhi ya waombolezaji kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ waliofika leo kuuaga mwili wa marehemu Brigedia Jenerali Cyril Ivor Mhaiki
 Waombolezaji mbali mbali na jamaa waliofika leo   kuuagawa  Mwili wa Marehemu Brigedia Jenerali Cyril Ivor Mhaiki.
 Jeneeza lenye Mwili wa Marehemu Brigedia Jenerali Cyril Ivor Mhaiki  aliyekua Kamanda wa Brigedi ya Nyuki Zanzibar, likibembwa kwenda sehemu maalumu ya kuagwa leo
 Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Viongozi pamoja na Wazee wa Chama wakiwa katika shughuli ya kuaga mwili wa marehemu Brigedia Jenerali Cyril Ivor Mhaiki 
 ​Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein  akitoa heshima ya mwisho
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein  alipokuwa ​akitoa mkono wa pole kwa wanafamilia wa Marehemu Brigedia Jenerali Cyril Ivor Mhaiki (Picha na Ikulu.)

0 comments:

Post a Comment

Mdau, Uwanja huu ni wako, Toa maoni yako yasaidie kujua wewe unafikiri nini kifanyike kuboresha zaidi maisha ya Watanzania. Maoni yako yasilenge kuchochea mtafaruku katika jamii, kisiasa, kidini, kikabila au kijinsia. Mawasiliano yetu:- simu +255 (0) 712 498008, Email: nkoromo@gmail.com.
Bashir Nkoromo
Msimamizi Mkuu, Blog ya Taifa ya CCM.