Thursday, December 15, 2016

KINANA AZINDUA JENGO LA KISASA LA KITEGAUCHUMI LA CCM, UPANGA JIJINI DAR ES SALAAM, LEO

Jengo la kisasa la Kitegauchumi la Chama Cha Mapinduzi (CCM), lilipo Upanga jijini Dar es Salaam, lililozinduliwa leo na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, Abdulrahman Kinana. 

Kwa mujibu wa maelezo ya Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini wa Mali za Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mama Anna Abdallah, ujenzi wa jengo umegharimu sh. Bilioni saba.

Mama Anna Abdallah, amesema, jengo hilo limejengwa kwa hali ya juu na limewekwa kila kitu ikiwemo zamani.

"Mpangaji anapotaka kuingia katika nyumba hii, yeye anachopaswa kufanya ni kuja na chakula na nguo tu, halazimiki kuingia na zamani ya yoyote hata TV anaikuta ipo sebuleni", Alisema, Mama Anna.
 Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha Zakia Meghji akizungumza wakati wa uzinduzi wa jengo la Kisasa la Kitegauchumi la CCM, lilipo Upanga jijini Dar es Salaam, leo.
 Baadhi ya waalikwa wakiwa kwenye hafla ya uzinduzi wa jengo la kisasa la kitegauchumi la CCM, Upanga jijini Dar es Salaam, leo. 
 Aliyekuwa Mratibu wa Kanda ya Pwani wa Chadema, na Baadaye Mratibu wa Kampeni wa ACT Wazalendo wakati wa uchaguzi Mkuu ulipita, Nixon Tugara akikabidhiwa kadi ya CCM na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alipoamua kuhamia CCM wakati wa uzinduzi wa jengo la Kitegauchumi la CCM, Upanga jijini Dar es Salaam, leo.
 Nixon Tugara akifurahia kadi yake ya CCM baada ya kukabidhiwa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana wakati wa hafla ya uzinduzi wa jengo la Kitegauchumi la CCM, Upanga jijini Dar es Salaam, leo
 Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini wa mali za CCM, Mama Anna Abdallah, akizungumza wakati wa uzinduzi wa jengo la Kisasa la Kitegauchumi la CCM, lilipo Upanga jijini Dar es Salaam, leo. 
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza kabla ya kuzindua jengo la Kitegauchumi la CCM, Upanga jijini Dar es Salaam, leo. 
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimpokea mwanachama mpya aliyejiunga na CCM kutokea Chadema, wakati wa hafla hiyo
 Tugara ambaye ni miongozi mwa watu waliosimamia ujenzi wa jengo hilo la Kitegauchumi akizungumza yaliyomsibu hadi kuhamia CCM, kutoka ACT Wazalendo na Chadema.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdultrahman Kinana akimshukuru Tugara kwa kuwa miongoni mwa viongozi waliosaidia katika kufanikisha ujenzi wa jengo la Kitegauchumi la CCM, lililopo Upanga jijini Dar es Salaam, ambalo amelizindua leo. Kulia ni Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha, Zakia Meghji.
 Tugara akimshukuru Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwasalimia baadhi ya wanachama wa CCM wakati akienda kuzindua jengo la Kitegauchumi la CCM, lililopo Upanga jijini Dar es Salaam, leo. Kushoto ni Mama Zakia Meghji
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizindua jengo la kisasa la Kitegauchumi la CCM, Upanga jijini Dar es Salaam, leo. Kushoto ni Mama Zakia Megji na Mama Anna Abdallah.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akikata utepe kuzindua rasmi jengo hilo. Kushoto kwake ni Mama Anna Abdallah na kulia kwake ni Mama Zakia Meghji.
 Katibu Mkuu wa CCM, Andulrahman Kinana akienda kukagua ndani ya jengo
 Kinana akitazama ukumbi wa mikutano katika jengo hilo
 Kinana akisalimiana na mmoja wa wajumbe wa Baraza la Wadhamini wa mali za CCM wakati akikagua jengo.


Samani ndani ya jengo
🔻

 jikoni

  
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiagana na viongozi kabla ya kuondoka baada ya kuzindua rasmi jengo la kitegauchumi la CCM, Upanga, Dar es Salaam, leo. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO-CCM Blog
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.