KIMBEMBE CHA KESI YA MBUNGE WA ARUSHA MJINI GODBLESS LEMA CHAENDELEA LEO

MAHAKAMA KUU KANDA YA ARUSHA YASIKILIZA RUFANI ZA PANDE ZOTE, LEO, AREJESHWA RUMANDE TENA
Arusha, Tanzania
Mahakama Kuu Kanda ya Arusha leo, imesikiliza maombi ya fufani ya upande wa Jamhuri na ule wa Mshitakiwa, Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, ambapo pande zote wamekubaliana kusikilizwa rufani ya  upande wa Jamhuri ambao umeiomba Mahakama kuwasilisha hati ya maandishi, Desemba 30,  2016.

Rufani hizo ambazo ni pamoja na ile ya upande wa jamhuri kutoridhika na maamuzi ya Jaji Modesta Opiyo la kuwapa siku kumi upande wa mshitakiwa Lema kufaili notisi ya rufaa ya upande wa mshitakiwa ni ile ya kupinga uamuzi wa mahakama ya chini kushindwa kumpa Lema masharti ya dhamana.

Jaji aliyekuwa anasikiliza kesi ya rufaa hizo, Salma Magimbi amesema kuwa baada ya upande wa Jamhuri kuleta rufaa kwa njia ya maandishi upande wa mshitakiwa Lema wataijibu, Desemba 30, 2016,  ambapo  Januari 2, 2017 watakutana pande zote kwa ajili ya kufanya majumuisho na maamuzi ya rufani hiyo yatatolewa Januari 4, 2017.

Baada ya kusikiliza rufaa hizo Mahakama imeibua hoja na kuwapa kazi mawakili wa pande zote kuangalia kuwa notisi iliyowasilishwa na mahakama ya chini imekidhi mahatwa ya kisheria au la?

Wakili wa mshitakiwa  Peter Kibatala amesema, upande wao wameiomba mahakanma kusubirisha rufaa yao ili wasikilize kwanza rufaa ya upande wa jamhuri kwani rufaa zote zimegongana na zinaelekea sehemu moja.

Lema amerudishwa rumande kusubiri maamuzi yatakayotolewa na mahakama.

0 comments:

Post a Comment

Mdau, Uwanja huu ni wako, Toa maoni yako yasaidie kujua wewe unafikiri nini kifanyike kuboresha zaidi maisha ya Watanzania. Maoni yako yasilenge kuchochea mtafaruku katika jamii, kisiasa, kidini, kikabila au kijinsia. Mawasiliano yetu:- simu +255 (0) 712 498008, Email: nkoromo@gmail.com.
Bashir Nkoromo
Msimamizi Mkuu, Blog ya Taifa ya CCM.