GARI LA MBUNGECWA CHADEMA LAUA MWANANCHI MBEYA LEO

Na JamiiMojaBlog,Mbeya
Mkazi wa Iyunga jijini Mbeya ambaye amefahamika kwa jina moja la Rechal, amefariki dunia baada ya kugongwa na gari , la Mbunge wa Mbeya Mjini kwa tiketi ya Chadema,  Joseph Mbilinyi aka Sugu.

Habari zilzizosambazwa na mwandishi wa Blog ya Jamii Moja ya Mbeya, (Jamii Moja Blog), zimedai kwamba tukio hilo limefanyika leo saa mbili asubuhi katika eneo la Iyunga mjini Mbeya.

Imedaiwa kuwa gari la Mbunge huyo, T161 CPP aina ya  Toyota LandCruiser ilimgonga mwenda kwa miguu huyo wakati akivuka kwenye eneo lenya alama ya kuvukia watembea kwa miguu (Zebra Cross), na kwamba mtembea kwa miguu huyo baada ya kugongwa alikufa papo hapo.

Mwandishi huyo amedai kuwa gari hilo la Sugu, lilikuwa katika mwendo kasi, linakwenda uwanja wa ndege wa Songwe kwa ajili ya mapokezi ya kiongozi wa Kitaifa Freeman Mbowe.

Amesema, Rechel akiwa katikati ya barabara marehemu alishangaa kuliona gari ya Mbunge hiyo likija kwa kasi kubwa hivyo kumuachia mkono na yeye kutafuta njia ya kujiokoa.

0 comments:

Post a Comment

Mdau, Uwanja huu ni wako, Toa maoni yako yasaidie kujua wewe unafikiri nini kifanyike kuboresha zaidi maisha ya Watanzania. Maoni yako yasilenge kuchochea mtafaruku katika jamii, kisiasa, kidini, kikabila au kijinsia. Mawasiliano yetu:- simu +255 (0) 712 498008, Email: nkoromo@gmail.com.
Bashir Nkoromo
Msimamizi Mkuu, Blog ya Taifa ya CCM.