Friday, November 25, 2016

RAIS DK MAGUFULI AZUMGUMZA LIVE KATIKA MKUTANO WA MAKONDA NA WANANCHI UBUNGO, ASEMA BOMOABOMOA HAINA MSALIE LABDA SHERIA IBADILISHWE

RAUS DK MAGUFULI
Na Bashir Nkoromo, Ubungo
RAIS Dk. John Magufuli ameeleza kufurahishwa kwake, na utaratibu wa Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, kwenda kwa wananchi kusikiliza kero.

Amesema, utaratibu huo wa kusikiliza kero ungefuatwa na viongozi wengi, hali ingekuwa tofauti na ilivyo sasa ambapo imefikia hatua wananchi wanakaa na kero bila kujua pa kuzipeleka.

"Nakupongeza sana Mheshimiwa Mkuu wa mkoa, kazi hii unayofanya ya kusikiliza kero za wananchi ni kazi nzuri sana. Natamani viongozi wote nchi nzima wangekuwa na utaratibu huu. Lakini viongozi wengi hawaende kwa wananchi, wanajifungia ndani", alisema, Rais Magufuli wakati akizungumza kwa simu ya Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Makonda aliweka sauti ya juu maongezi yake katika simu, ili kutoa ufafanuzi kuhusu mgogoro wa wananchi wa Ubungo na Tanroads, ambao uliibuliwa na mwananchi mmoja ambaye aliuliza swali kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika eneo la Maramba mawili, Mbezi, wilayani Ubungo.

Rais Magufuli alisema wananchi lazima waendelee kuelimishwa kwa sababu suala la hifadhi ya barabara ni la kisheria na hivyo ni lazima wazingatie. "Hivyo ndivyo sheria ilivyo, na kama wanaona haifai basi waombe ibadilishwe hata barabara ibaki mita mbili", alisema, Magufuli.

Amesisitiza kuwa bomoabomoa katika maeneo ya Ubungo itaendelea kuwepo, hasa wakati wa utekelezaji miradi ya uboreshaji miundombinu.  " Tukianza mradi wa barabara za juu 'Intercharnge' pale ubungo , majemgo mengi tutayavunja bila fidia hata likiwala Tanesco", alisema Rais Magufuli.

Magufuli alimtaka Makonda na Mkuu wa wilaya ya Ubungo Humphrey Polepole kuendelea kuchapakazi. "Nakuhakikishia Mheshimiwa Makonda, Nipo pamoja nawewe, endelea kuwatumbua hukohuko", alisema Rais Magufuli.

Makonda alifanya mkutano wa hadhara uliokuwa ukionyeshwa moja kwa moja na kituo kimoja cha Televisheni, ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake mkoa wa Dar es Salaam, ambapo tayari ameshapita katika  wilaya za Kigamboni, Temeke na Ilala.
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.