Sunday, November 13, 2016

HOTUBA YA WAZIRI MKUU WAKATI AKIHAIRISHA SHUGHULI ZA MKUTANO WATANO WA BUNGE LA 11 MJINI DODOMAwA

Waziri Mkuu Majaliwa
1. Mheshimiwa Spika, awali ya yote, naomba kutumia fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutulinda na kutufikisha salama siku ya leo tunapohitimisha Mkutano wa Tano wa Bunge lako Tukufu tuliouanza tarehe 1 Novemba, 2016.

2. Mheshimiwa Spika, nitumie fursa hii pia kukupa pole, kwa msiba mzito uliotokea tarehe 7 Novemba, 2016 ambao Bunge lako tukufu, Serikali na Taifa tumepata kwa kumpoteza Mheshimiwa Samwel Sitta, mmoja wa Viongozi mahiri wa Bunge hili katika historia ya nchi yetu. 

Msiba uliotupata wa aliyekuwa Spika Mstaafu wa Bunge la Tisa (2005-2010) na Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Urambo Mkoani Tabora ni pigo kwa Taifa letu. Nasi Wabunge kwa kuwawakilisha Watanzania leo hii muda mfupi ujao tutaaga mwili wa kipenzi chetu Mheshimiwa Samuel Sitta. Tunamwomba Mwenyezi Mungu ailaze Roho ya Marehemu mahali pema Peponi. Amina.

3. Mheshimiwa Spika, naomba nitumie fursa hii kutoa pole kwa mjane wa marehemu, Mheshimiwa Margareth Simwanza Sitta../INAENDELEA
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.