Monday, November 14, 2016

DONALD TUMP AANZA KUTEUA, AMETEUA MWENYEKITI WA KAMATI YA TAIFA YA CHAMA CHA REPUBLICAN KUWA MKUU WA WAFANYAKAZI

Marekani
Reince Priebus alionekana na Donald Trump usiku wa siku ya uchaguzi.

Rais mteule wa Marekani, Donald Trump, amemteua Mwenyekiti wa kamati ya taifa ya chama cha Republican, Reince Priebus, kuwa mkuu wa wafanyakazi.

Bwana Priebus ana uhusiano wa karibu na spika wa baraza la wawakilishi Paul Ryan. 

Wandishi wa wa habari wanaarifu kwamba uteuzi wa Piebus unaweza kuwaudhi wafuasi wake wa hali ya chini na hii inaashiria kwamba uongozi ujao unalenga kufanya kazi kwa karibu na baraza la Congress kujihakikishia ushindi wa mapema wa baraza hilo.
Marekani
Stephen Bannon aliacha kazi yake ya awali na kuwa kampeni meneja wa Donald Trump.

Stephen Bannon, alikuwa ni mwenyekiti wa taasisi ya Breitbart News, ambayo ni tovuti yenye maoni ya mrengo wa kulia , naye ameteuliwa kwa nafasi ya mkuu wa mipango na mshauri mwandamizi.

Mkuu wa wafanyakazi ambaye anafanya kazi kama mruhusu na mtengeneza ajenda kwa rais, na kwamba ni mmoja wa chaguo muhimu la mapema kwa rais ajae.

Katika taarifa yake, Trump alinukuliwa akiwazungumiza Priebus na Bannon ni viongozi wenye sifa za hali ya juu waliofanya kazi pamoja wakati wa kampeni zake za kuingia Ikulu ya Marekani.BBC
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.