Monday, November 28, 2016

COMRADE FIDEL CASTRO: KIONGOZI KEKEE WA DUNIA ALIYEACHA URITHI WA VITU VIWILI KWA KILA RAIA WA NCHI YAKE

.
Ndugu zangu,
Dunia itamkumbuka Fidel Castro. Afrika itamkumbuka sana Fidel Castro, lakini, watu wa Cuba watamkumbuka zaidi Fidel Castro.


Mwanamapinduzi Fidel Castro ni kiongozi pekee wa dunia ambaye, alihakikisha mapinduzi ya Cuba yazae matunda kwa Wa-Cuba.


Baada ya Mapinduzi, Fidel Castro alihakikisha na ikawa hivyo, kuwa kila m-Cuba anayezaliwa, atakuwa na hakika ya kupata mambo mawili muhimu bila kulipia hata senti tano, kwa maisha yake yote; Afya na Elimu. Na vyote hivyo, ni kwa ubora.


Comrade Fidel Castro amekufa akiacha urithi huo muhimu kwa watu wake.


Fidel Castro aliipenda Afrika pia. Alitaka viongozi wetu wafuate mfano wa Cuba. Walipokwama Comrade Castro aliwasaidia. Misaada yake mikubwa ilikuwa kwenye Afya na Elimu.


Ndio maana, hata madaktari wetu wengi wamesomea Cuba. Ndio maana, tangu miaka ya 70, tumekuwa na shule mbili za Sekondari za kilimo zilizojengwa na kufadhiliwa vifaa na Serikali ya Cuba. Ni Sekondari za Kibiti na Ruvu. Nyingine au vingine nilivyovisahau nikumbusheni Mwenyekiti wenu!
Viva El Commandante Fidel Castro!
Maggid, 0688 37 36 52/ 0754 678 252
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.