Sunday, October 16, 2016

WAFANYAKAZI NEW HABARI CORPORATION HATARINI KUWA VIZIWI.  MKURUGENZI WA MANISPAA YA UBUNGO MH. JOHN KAYOMBO   
Na Nassir Bakari 
 
Ziara ya ghafla iliyofanywa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Mh. John Kayombo imefichua mambo mengi likiwemo kelele zisizo za kawaida zinazotolewa na mtambo wa kutengeneza magazeti katika kampuni ya New Habari Corporation zinazohatarisha uwezo wa kusikia wa wafanyakazi.

Hatua ya Mkurugenzi kutembelea hapo imekuja muda mfupi baada ya kusikia vilio vya wananchi na wafanyabiashara wanaoishi jirani na kiwanda hiko.

Mkazi mmoja anayefanya biashara karibu na eneo hilo amesema muda mrefu wametoa malalamiko yao lakini hayakufanyiwa kazi, wakaamua kumfikishia kiongozi shupavu, mwenye nia ya dhati ya kuwatumukia wananchi Mh. John Kayombo.

Baada ya malalamikio ya wananchi kumfikia, bila kupepesa macho Mkurugenzi  Kayombo akaenda  New House Corporation bila kutoa taarifa kwa uongozi wa kiwanda kwa nia ya kwenda kuona hali halisi.

Akiwa kiwandani hapo Mkurugenzi Kayombo alikagua maeneo mbalimbali yanazonguka kiwanda na hatimaye akafika kwenye mashine ya kutengeneza magazeti yanayotolewa na kampuni hiyo .
 
Mashine hiyo ilikuwa inapiga kelele hali ambayo sio rahisi kwa binadamu kukaa eneo hilo lakini alikuta wafanyakazi wakiwa hapo tena bila kifaa chochote cha kuzuia ama kupunguza sauti hizo.
 
Baada ya kuona hali hiyo Mkurugenzi Kayombo alisema sio vizuri kuona binadamu tukitesana wenyewe kwa namna mbalimbali .

“Hili jambo sio zuri, haiwezekani mashine ipige kelele kiasi hiki huku wafanyakazi wakiendelea kuzalisha magazeti, huu ni ukatili na ni kwenda kinyume na haki za binadamu,” alisema Mkurugenzi na kuendelea:-

“Hii hali ikiendelea itasababisha wafanyakazi wengi kupoteza uwezo wa kusikia hatimaye kushindwa kufanya kazi za kujenga Taifa,” alisema Mkurugenzi Kayombo.

Pia Mkurugenzi Kayombo alisema Kiwanda hicho kujitadhimini katika utendaji wa kazi na kuhakikisha wanapunguza ama kuondoa kabisa kelele zinazotolewa na mashine hiyo.


Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.