Sunday, October 2, 2016

RAIS DK. MAGUFULI ATEUA MWENYEKITI MPYA BODI YA SHIRIKA LA BIMA LA TAIFA

Rais  Dk. Magufuli
Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli, leo tarehe 02 Oktoba, 2016 amemteua Laston Thomas Msongole kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Bima la Taifa (NIC).

Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu jijini Dar es Salaam, imesema  Laston Thomas Msongole anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dk. Edmund Mndolwa ambaye amemaliza muda wake.

"Uteuzi wa Laston Thomas Msongole umeanza leo tarehe 02 Oktoba, 2016", imesema taarifa hiyo ya Ikulu iliyosaininiwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, GersonMsigwa.
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.