Friday, September 30, 2016

WATEJA BAYPORT WAANZA KUPEWA HATI KILWA

Afisa Sheria wa Bayport Financial Services, Mrisho Mohamed katikati akimkabidhi hati yake ya kiwanja mteja wao aliyenunua kiwanja cha Kilwa, Mubarack Kirumirah kulia. Kushoto ni Mratibu wa Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Mercy Mgongolwa.


Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
WATEJA wa viwanja vya Bayport Financial Services wilayani Kilwa, mkoani Pwani wameanza kupewa hati zao kutoka mradi wa Kilwa Msakasa unaoendeshwa na taasisi hiyo inayojihusisha na mikopo, huku ikiwa na dhamira ya kuwakwamua wateja wao na Watanzania kwa ujumla.

Mradi wa Kilwa Msakasa ni miongoni mwa miradi kadhaa inayoendeshwa na taasisi hiyo ikiwamo Bagamoyo, Vikuruti, Kigamboni na Kibaha na kujikita kurahisisha pia utoaji wa hati kwa wateja wao waliokamilisha utaratibu rahisi wa malipo ya viwanja hivyo.Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mratibu wa Masoko na Mawasiliano, Mercy Mgongolwa, alisema kwamba kuanza kutolewa kwa hati za mradi huo wa Kilwa ni sehemu ya mwendelezo wa kuboresha huduma zao za mikopo ya viwanja inayotolewa sehemu mbalimbali nchini Tanzania.
Mteja wa Bayport Financial Services, Mubarack Kirumirah kulia akitia sahihi kabla ya kukabidhiwa hati yake ya kiwanja cha Kilwa. Anayeshuhudia ni Afisa Sheria wa Bayport Financial Services, Mrisho Mohamed.
Shughuri za maandiko ya kukabidhiana hati zikiendelea katika ofisi za Bayport jana.


Alisema taasisi yao imeendelea kuboresha huduma zao ili kuhakikisha kwamba kila Mtanzania anapata uwezo wa kumiliki kiwanja chenye hati kwa ajili ya kuvitumia katika mipangilio ya maisha yao.

“Bayport ni taasisi ambayo imekusudia kuona watu wanamiliki viwanja vyenye hati kwa urahisi, hivyo kila aliyekopa kiwanja au kununua kwa fedha taslimu kupitia kwetu atakabidhiwa hati yake haraka iwezekanavyo kwa sababu tumedhamiria kuwakwamua wateja wetu wote, hivyo wale ambao hawajapata fursa ya kuhudumiwa na ofisi yetu wafanye hivyo ili waone namna gani Bayport ipo kwa ajili yao,” alisema Mercy.

Naye Afisa Sheria wa Bayport Financial Services, Mrisho Mohamed, aliwataka wateja wao kutembelea katika ofisi za taasisi yao zilizoenea nchi nzima ili wapate huduma bora za mikopo ya viwanja inayowahusu watumishi wa umma, wafanyakazi wa kampuni binafsi pamoja na wajasiriamali.

“Tunajivunia kufanya kitu tofauti kwa wateja wetu ndio maana kila anayepata kiwanja kwetu tunahakikisha kwamba hapati usumbufu wowote wa kufuatilia hati sehemu husika badala yake sisi ndio tumechukua jukumu hilo tukiamini kwamba jambo hili litakuwa mkombozi kwa wateja wote,” alisema Mohamed.

Naye mteja wa Bayport aliyekabidhiwa hati yake ya kiwanja cha Kilwa, Mubarack Kirumirah Hamidu, aliwashukuru Bayport kwa kufanya kazi nzuri inayowaendelea usumbufu wateja wao kufuatilia hati za viwanja, jambo linaloonyesha utofauti mkubwa katika suala zima la ardhi.

“Nashukuru kwa kupata hati ya kiwanja change kwa kipindi kisichozidi miezi mitatu tangu nilipojitokeza kununua kiwanja cha Kilwa Msakasa, hivyo suala hili limenifurahisha na kuwaeleza Watanzania wenzangu kuchangamkia kununua viwanja vya Bayport,” alisema.

Wengine waliokabidhiwa hati zao za viwanja vya Kilwa ni Mrina Harish Mawji, Jigar Patel, Amina Haidari Amani, Victoria Ambrose Kundi na wengine wengi ambao wamekuwa miongoni mwa Watanzania waliojitokeza kwa wingi kuchangamkia fursa ya mikopo ya viwanja vya Bayport vinavyoendelea kutolewa na taasisi hiyo nchini Tanzania.
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.