LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 26, 2016

WAZIRI DK. MAHIGA KUWASILISHA VIPAUMBELE VYA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA BARAZA KUU LA 71 LA UMOJA WA MATAIFA

Na Mwandishi Maalum, New York
Waziri  wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki , Dk. Augustine Mahiga, leo atapata fursa ya kueleza vipaumbele vya Tanzania, atakapokuwa akitoa hotuba katika Mkutano wa Baraza Kuu la 71 la Umoja wa Mataifa ulioanza wiki iliyopita jijini New York, Marekani.

Waziri Dk. Mahiga, anapata fursa hiyo wa viongozi wakuu wa Nchi na Serikali, kutoka mataifa mbalimbali Duniani, katika mkutano huo, wamepewa fursa za kuleleza vipaumbele vya nchi zao.

Katika kueleza vipaumbele mambo makubwa ambayo  karibu kila kiongozi ameyagusia katika  hotuba  yake ni  pamoja na  tatizo la kuongezeka kwa matukio ya  ugaidi,  tatizo la  wakimbizi na  wahamiaji, vita na machafuko vinavyoendelea katika nchi  kadhaa,  ubaguzi kwa misingi ya  dini au eneo analotoka mtu, mabadiliko ya tabia nchi na utekelezaji wa malengo mapya ya maendeleo endelevu.

Pamoja na viongozi hao  kushiriki katika majadiliano ya  jumla ya Baraza Kuu, lakini pia  wamekuwa  wakishiriki mikutano mingine ya pembezeni ambayo imeandaliwa sambamba na  mkutano mkuu.

 Aidha   mikutano ya kimataifa na mikubwa kama huu wa 71 wa Baraza Kuu pia hutumika na viongozi  wakuu na  wa nchi na serikali kama  sehemu ya kukutana na kufanya mazungumzo  na kuweka mikakati ya  mahusiano baina  ya nchi zao.

TASWIRA MKUTANO WA BARAZA KUU LA UMOJA WA MATAIFA LA 71
Waziri Mahinga  alipoongoza kikao  cha Troika ya  SADC
Waziri Dk Mahiga, alipokutana na kufanya mazungumzo na  Naibu  Waziri Mkuu na Waziri wa  Ushirikiano wa Maendeleo wa Belgium   Bw. Alexander De Croo
Waziri  Mahinga akibadilishana  mawazo na   Waziri wa  Mambo  ya Nje wa  Sultanate of Oman, Bw. Yusuf bin Alawi bin Abdullah
Waziri  wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa  Afrika Mashariki akiwa katika  Mkutano wa Mawaziri wa  Nje wa  nchi za Jumuiya ya Madola.
Diplomasia ya  Corridon,  Hapa  Waziri  wa Mambo ya Nje  na Ushirikiano a Kimataifa,  akiwa na ujumbe wa Morocco
Waziri katika Mazungumzo na  Waziri wa  Mambo ya Nje wa Kuwaiti, Sabah Al KHalid Ala Sabah

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages