RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE AHUTUBIA MAELFU YA WAKAZI WA JIJI LA NEW YORK MAREKANI NA KUSISITIZA UMUHIMU WA ELIMU

 Kamishna wa Kamisheni ya Kimataifa ya Elimu, Rais Mstafu Jakaya Kikwete, akihutubia maelfu ya wananchi katika jiji la  New York, Marekani, wakati wa tamasha la 'Global Citizen Festival' lililofanyika Central Park. Kikwete aliitaka Jumuiya ya kimataifa kuchangia na kuwekeza katika elimu kwa  mustakabali wa kizazi  cha sasa na kijacho. Kulia ni Makamishna mwenzake, Waziri Mkuu wa Norway Erna Solberg
Umati wa  wakazi wa jiji na  New York waliojitokeza katika  tamasha hilo fedha zinazopatikana kipitia  tamasha hilo  hupelekwa kusaidia masuala mbalimbali ya kijamii. Tamasha hilo lilitumbuizwa na wanamziki maafuru akiwamo Rihanna ambaye ametangazwa kuwa Balozi wa  Elimu
Rais Mstaafu akibadilishana mawili matatu na  Waziri wa  Mazingira wa Nigeria   Amina Mohammed ambaye naye alikuwa mmoja  wazungumzaji katika tamasha hilo
Rais Mstaafu Kikwete  akisalimiana na  Balozi wa  Marekani katika Umoja wa Mataifa,  Samantha  Power  walipokutana kwenye tamasha hilo

0 comments:

Post a Comment

Mdau, Uwanja huu ni wako, Toa maoni yako yasaidie kujua wewe unafikiri nini kifanyike kuboresha zaidi maisha ya Watanzania. Maoni yako yasilenge kuchochea mtafaruku katika jamii, kisiasa, kidini, kikabila au kijinsia. Mawasiliano yetu:- simu +255 (0) 712 498008, Email: nkoromo@gmail.com.
Bashir Nkoromo
Msimamizi Mkuu, Blog ya Taifa ya CCM.