Wednesday, September 21, 2016

RAIS MAGUFULI AMWONDOA MWENYEKITI BODI YA UDHAMINI YA MFUKO WA PENSHENI WA LAPF

RAIS MAGUFULI
Dar es Salaam
Rais Dk. John Magufuli, leo tarehe 21 Septemba, 2016 ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Udhamini ya Mfuko wa Pensheni wa LAPF Prof. Hasa Mlawa kuanzia leo.

Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu, jijini Dar es Salaam, imesema pamoja kutengua uteuzi wa Prof. Hasa Mlawa, Rais Magufuli amevunja Bodi ya Udhamini ya Mfuko huo.

Taarifa hiyo imekamilisha kwa maelezo kwamba uteuzi wa Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Udhamini ya LAPF utafanywa baadaye.

Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.