RAIS JOHN MAGUFULI KUZINDUA KESHO NDEGE MPYA ZA ATC

Na Lilian Lundo-MAELEZO
Rais Dk. John Magufuli kesho anatarajiwa kuzindua ndege mbili za Shirika la Ndege la Tanzania (ATC) zilizonunuliwa kwa kutumia kodi za wananchi.

Uzinduzi huo unatarajiwa kufanyika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (Terminal 1).

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu (Uchukuzi), Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Dk. Leonard Chamuriho leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uzinduzi wa ndege hizo.

Dk. Chamuriho alisema kuwa ndege ya kwanza iliwasili nchini tarehe 20/09/2016 na ndege ya pili ilitarajiwa kuwasili nchini leo tarehe 27/09/2016 kuanzia saa 6:00 mchana.

Vile vile Katibu Mkuu huyo alisema kuwa ndege hizo zimenunuliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kuhudumia wananchi wa ndani ya nchiya Tanzania na nchi jirani.

“Ndege hizo aina ya Dash 8 Q400 zimetengenezwa na kiwanda cha Bombadier nchini Canada ambapo kila moja ina uwezo wa kubeba abiria 76 na zitatumika katika kuhudumia soko la ndaniya Tanzania na nchi jirani,” alifafanua Dkt. Chamuriho.

Aidha, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inawakaribisha wananchi wote kushuhudia uzinduzi wa ndege hizo unaotarajiwa kuanza saa mbili kamili (2:00) asubuhi.

1 comment: Leave Your Comments

 1. SALAAM ZA PONGEZI KWA RAIS WANGU JOHN POMBE MAGUFULI.

  Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa dhati Kabisa kama Kijana & Kada mtiifu wa Chama Cha Mapinduzi ninaetambua juhudi/Jitihada zako unazozionyesha kila siku iitwapo leo za kuwaletea Maendeleo Wananchi wako napenda kukupongeza kwa Kutimiza Ahadi yako ya kufufua Shirika la Ndege la Taifa " ATCL" kwa kununua Ndege Mbili Mpya na leo tumepokea Ndege ya Pili.

  Sasa Watanzania Wote wamejionea wenyewe na Ulimwengu umejionea wenyewe ya Kwamba Tanzania Mpya yaja.

  Mheshimiwa Rais Hongera sana na Mungu akubariki, Akulinde na kukujaalia Afya njema ili ukatimize vyema Majukumu yako ya kuwatumikia Watanzania kwa Kuwaletea Maendeleo.

  Robert PJN Kaseko
  Mjumbe Baraza Kuu UVCCM Mkoa wa Arusha
  September 27, 2016.

  ReplyDelete

Mdau, Uwanja huu ni wako, Toa maoni yako yasaidie kujua wewe unafikiri nini kifanyike kuboresha zaidi maisha ya Watanzania. Maoni yako yasilenge kuchochea mtafaruku katika jamii, kisiasa, kidini, kikabila au kijinsia. Mawasiliano yetu:- simu +255 (0) 712 498008, Email: nkoromo@gmail.com.
Bashir Nkoromo
Msimamizi Mkuu, Blog ya Taifa ya CCM.