Thursday, September 29, 2016

RAIS DK MAGUFULI: SERIKALI ITANUNUA NDEGE MPYA AINA YA JET

Na Sheila Simba, Dar es Salaam
RAIS  John Magufuli amesema Serikali imejipanga kununua ndege mbili  aina Jet zenye uwezo wa kubeba abiria 160 na 242 pamoja na kutenga Tsh. Bilioni 100 kwa ajili ya ukarabati
viwanja vya ndege nchini.

Amesema hayo leo Jijini Dar Es Salaam wakati wa uzinduzi wa ndege mpya mbili za abiria aina ya  bombardier – 8 Q400 zilizonunuliwa na Serikali kutoka nchini Canada, na uongeza kuwa ndege hizo zitasaidia kuboresha sekta ya usafiri wa anga nchini.

“Ndege hizi ni nzuri sana, kwani ukitaka kujenga nchi yenye uchumi wa kisasa huwezi kujenga bila kuwa na ndege na ukitaka watalii lazima uwe na ndege” alisema Rais Magufuli

Alisema  kuwa ndege hizo mbili zitakazonunuliwa na

Serikali zitakuwa na uwezo wa kubeba kusaidia watalii kuja nchini moja kwa moja bila kutua nchi nyingine.

“Tunataka watalii wanaokuja nchini kuja moja kwa moja bila kushuka nchi nyingine ili kuongeza mapato yetu na kukuza utalii duniani na kuwa na ndege nyingi zaidi kama nchi nyingine” alisema Rais Magufuli.

Akizungumzia ubora wa ndege za Bombardier alisema kuwa ndege hizo zinaenda na mazingira ya hapa nchini na zina
uwezo wa kutua katika viwanja vyenye lami na vile ambavyo havina lami na uendeshaji wake ni wa gharama nafuu.

Kwa mujibu wa Rais Magufuli alisema kuwa ndege za bombardier zinatumia mafuta kidogo ikiwemo gharama ya sh Milioni 1 za mafuta kwa safari moja ikilinganisha na ndege nyingine zenye kutumia tsh. Milioni 28 kwa safari.

Rais Magufuli aliitaka bodi ya shirika la ndege Tanzania (ATCL) kufanya kazi nzuri ya kusimamia ndege hizo na
kutoa huduma nzuri na kuhakikisha wanapata faida ili serikali waweze kununua ndege nyingi zaidi.

Alisema kuwa bodi ya ATCL wana kazi kubwa ya kufanya kuboresha shirika hilo, kutokana na uzembe wa wafanyakazi
wake kutokuwa makini na kuwataka kupanga vizuri safari za ngede hizo kwani zina uwezo wa kwenda mpaka nchi jirani.

“lazima mjue mnaingia kwenye ushindani na washindani wenu hawawezi kufurahia wapo hujuma ili shirika lisisonge mbele sasa fanyeni kazi”alisema Magufuli.

Aidha amewaomba ATCL kutotumia mawakala katika kukatisha tiketi na kuzingatia muda wa safari ulipangwa na
kutoa huduma nzuri kwa wateja wao ili kukuza utalii nchini  na kuwaomba watanzania kuwa wazalendo kwa kutumia usafiri huo.

Kwa upande wake Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa alisema ndege hizo
zilizozinduliwa zinauwezo wa kubeba abiria 76 na abiria 6 wakiwa ni wa daraja la biashara na 70 ni daraja la kawaida na ina uwezo wa kubeba mzigo wa tani moja.

Ameongeza kuwa shirika la ATCL lina upungufu mkubwa wa watalaamu katika maeneo mbalimbali ikiwemo, marubani,
wahandisi, wanasheria, maafisa biashara, wahasibu na menejimenti na hatua inayosabisha shirika hilo kushindwa kujiendesha vizuri.

Waziri Mbarawa alisema kuwa ATCL wamejipanga kutoa huduma za usafiri katika viwanja vya Dodoma, Dar Es Salaam, Bukoba, Tabora, Zanzibar, Mbeya, Kilimanjaro, Mtwara, Mwanza Kigoma, Arusha na Comoro.  

Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.