NUKUU ZA RAIS JOHN POMBE MAGUFULI-04

Na Nassir Bakari

Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Mheshimiwa John Pombe Magufuli, ni kiongozi ambaye watanzania tulikuwa tunamsubiri kwa muda mrefu.Mara nyingi anapohutubia huwa anatoa kauli za kufurahisha kwa wapenda maendeleo na kuchukiza wasiopenda maendeleo.
Mtandao huu unakuletea Nukuu za Rais, ambazo zinafurahisha wengi na kuchukiza wachache.

NUKUU

"Nataka niwaeleze ndugu zangu, serikali hii ya awamu ya tano ipo pamoja nanyinyi, haitowatupa wala haitowabagua, haitowabagua kwa dini zenu haitowabagua kwa makabila yenu na kamwe haitowabagua kwa sababu ya vyama vyenu."

MAANA YAKE

Serikali ipo kwa ajili ya kutenda haki kwa raia wote bila kujali dini, kabila au vyama.

Maneno hayo alisema Magomeni, alipowatembelea wakazi waliokuwa wakiishi magomeni kota. Jumanne,06 Septemba, 2016. 

MUANDAAJI. NASSIR BAKARI
OFISI NDOGO ZA CCM
LUMUMBA 
EMAIL: nassiribakari@gmail.com0 comments:

Post a Comment

Mdau, Uwanja huu ni wako, Toa maoni yako yasaidie kujua wewe unafikiri nini kifanyike kuboresha zaidi maisha ya Watanzania. Maoni yako yasilenge kuchochea mtafaruku katika jamii, kisiasa, kidini, kikabila au kijinsia. Mawasiliano yetu:- simu +255 (0) 712 498008, Email: nkoromo@gmail.com.
Bashir Nkoromo
Msimamizi Mkuu, Blog ya Taifa ya CCM.