NUKUU ZA RAIS JOHN POMBE MAGUFULI-02NA NASSIR BAKARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani, Mheshimiwa John Pombe Magufuli ni kiongozi ambaye watanzania tulikuwa tunamsubiri kwa miaka mingi.

Mara nyingi anapohutubia huwa anatoa kauli ambazo zinafurahisha kwa wapenda maendelo na zinachukiza kwa wasiopenda maendeleo, mtandao huu unakuletea Nukuu za Rais ambazo zinawafurahisha wengi na kuwachukiza wachache.

NUKUU

"Ndani ya miezi miwili tutaanza kujenga majengo na majengo ya mwanzo yatakayojengwa ni haya ya wakazi 644 na yakapomalizika kujengwa, watakabidhiwa nyumba hizo  kwa sababu kuanzia mwaka 2012 mlikuwa mnapanga nyumba mpaka zikikamilika mwakani mtakuwa mmefikisha miaka mitano, hiyo miaka mitano mtakaa kwenye nyumba hizi hakuna kulipa.  Baada ya hiyo miaka mitano,  tutajenga utaratibu wa hizo nyumba mtakazokuwa mmekaa  muuziwe na tutawauzia kwa bei ya kawaida ya chini."

Maneno hayo aliyasema  Magomeni, alipowatembelea wakazi waliokuwa wakiishi magomeni kota. Jumanne,06 Septemba, 2016. 

MUANDAAJI.
NASSIR BAKARI
OFISI NDOGO ZA CCM,
LUMUMBA.
PHONE:0713 311 300
EMAIL.nassiribakari@gmail.com

0 comments:

Post a Comment

Mdau, Uwanja huu ni wako, Toa maoni yako yasaidie kujua wewe unafikiri nini kifanyike kuboresha zaidi maisha ya Watanzania. Maoni yako yasilenge kuchochea mtafaruku katika jamii, kisiasa, kidini, kikabila au kijinsia. Mawasiliano yetu:- simu +255 (0) 712 498008, Email: nkoromo@gmail.com.
Bashir Nkoromo
Msimamizi Mkuu, Blog ya Taifa ya CCM.