Tuesday, September 20, 2016

NDEGE YA KWANZA ILIYONUNULIWA NA SERIKALI YAWASILI NCHINI


NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
NDEGE moja mpya kati ya mbili zilizonunuliwa na Serikali na ambazo zilikuwa zikisubiriwa kwa hamu na Watanzania, imewasili nchini leo Septemba 20, 2016 kutoka nchini Canada.

Ndege hiyo ya abiria aina ya Bombadier Q400 NextGen, iliyotengenezwa na kampuni moja nchini Canada, imewasili majira ya mchana na kupokelewa kwa kunyunyuziwa maji, (Water Salutation), na magari mawili ya Kikosi cha zimamoto kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Akiipokea ndege hiyo kwa niaba ya Serikali, Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi, Ujezi na Mawasiliano, Dkt. Leonard Chamriho, amesema ndege ya pili inatarajiwa kuwasili baada ya wiki moja na kwamba baada ya kuwasili ndege ya pili ndipo yatafanyika mapokezi rasmi, yatakayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa tarehe itakayotangazwa baadaye.

Baada ya shughuli ya kuipokea ndege hiyo, ilipelekwa kwenye  maegeshwa ye ndege za jeshi (Airwing Ukonga).
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.