NAIBU WAZIRI TAMISEMI, SULEIMAN JAFO APATA AJALI YA GARI

Image result for picha ya jafo suleimani
MHESHIMIWA SULEIMAN JAFO
 Na Nassir Bakari

Mbunge wa jimbo la Kiasarawe na Naibu Waziri wa Tamisemi, Suleiman Jafo amepata ajali  ya gari eneo la Katela Kata ya Kiwira, Wilaya ya Rungwe Mbeya.

Ajali hiyo imehusisha gari dogo aina ta Corola iliyokuwa ikotokea Mbeya kwenda Rungwe na gari ya Naibu Waziri Selemani Jafo alikuwa akitokea Tukuyu kikazi.

Akizungumza na mtandao huu, Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya, Mariam Mtunguja alisema,katika gari aliyopanda mheshimiwa Jafo walikuwa watu watatu, Waziri Jafo, Katibu wake na Dereva na katika ajali hiyo iliyohusisha magari mawili hakukuwa na majeruhi wala mtu aliyefariki

"Katika gari aliyopanda mheshimiwa  Waziri walikuwa watu  watatu, Waziri Jafo, Katibu wake na Dereva,.baada ya kupata ajali hiyo walipelekwa Hospitali ya Mkoa wa Mbeya ambapo walifanyiwa uchunguzi kama wameumia kwa ndan au laa! Lakin bahati nzuri Daktari aliyewafanyia uchunguz alisema hakuumia popote ni wazima," alisema Katibu Tawala Mkoa,Mtunguja na kuendelea;-

" baada ya hapo Waziri na watu waliendelea na safari yao kuelekea mjini Dodoma kwa ajili ya kuwahi vikao vya Bunge."alisema Katibu Tawala Mkoa, Mtunguja
img-20160905-wa0062-1Gari la Naibu Waziri wa Tamisemi likionekana baada ya kugongwa katika ajali hiyo. img-20160905-wa0061Gari lililoigonga gari la Naibu Waziri likiwa limetupwa korongoni. img-20160905-wa0066img-20160905-wa0064-2Askari wa usalama barabaran wilaya Rungwe, Mbeya wakipima ajali ilivyotokea.

0 comments:

Post a Comment

Mdau, Uwanja huu ni wako, Toa maoni yako yasaidie kujua wewe unafikiri nini kifanyike kuboresha zaidi maisha ya Watanzania. Maoni yako yasilenge kuchochea mtafaruku katika jamii, kisiasa, kidini, kikabila au kijinsia. Mawasiliano yetu:- simu +255 (0) 712 498008, Email: nkoromo@gmail.com.
Bashir Nkoromo
Msimamizi Mkuu, Blog ya Taifa ya CCM.