LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 15, 2016

MATUKIO MBALIMBALI KUTOKA BUNGENI MJINI DODOMA JANA


 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi. Mhe. Mwigulu Nchemba akiwaeleza jambo Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (kushoto) na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi wakati wa kikao cha bunge kinachoendelea leo Mjini Dodoma.
 
 
 Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge,Kazi,Ajira na Walemavu Mhe. Anthony Mavunde akijibu swali wakati wa kikao cha bunge kinachoendelea leo Mjini Dodoma.


 Baadhi ya wageni waalikwa wakifuatilia mijadala bungeni leo

 Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina akijibu swali wakati wa kikao cha bunge kinachoendelea leo Mjini Dodoma ambapo alisema kuwa serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni mbili (2) katika mfuko wa mazingira kwa ajili ya zoezi ya upandaji miti ili kutunza mazingira.
 

 Waziri Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage  akijibu swali wakati wa kikao cha bunge kinachoendelea leo Mjini Dodoma ambapo alisema kuwa agizo la Rais Dkt. Magufuli la kuhakikisha viwanda vinavyobinafsishwa vinafanya kazi linaendelea kutekelezwa tangu Novemba 2015
 

 Mwenyekiti wa Bunge Mhe. Azzan Musa Zungu akiendesha kikao cha bunge leo mjini Dodoma

Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt. Charles Tizeba akiwasilisha bungeni Muswada wa Sheria ya Taasisi ya Utafiti wa Kilimo wa mwaka 2016

 Baadhiya wabunge wakiingia katika ukumbi wa Bunge kuhudhuria vikao vya bunge vinavyoendeleo Mjini Dodoma.

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages