MAKAMU WA RAIS MAMA SAMIA SULUHU HASSAN AZUSHIWA KUOMBA KUJIUZULU, OFISI YAKE YAKANUSHA VIKALI UZUSHI HUO

MAMA SAMIA
Dar es Salaam, Tanzania
Ofisi ya Makamu wa Rais imekanusha vikali kuwa taarifa inayosambazwa kwenye baadhi ya mitandao kuwa Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan ameomba kujiuzulu wadhifa wake,  ni ya uongo.

Taarifa ilyotolewa hivi punde leo, na Ofisi ya Makamu wa Rais, imesema, taarifa hiyo ni ya uzushi na uongo na kuomba wananchi kuipuuza mara moja kwa kuwa mbali ya kupotosha wananchi lakini pia ina lengo la uchochezi na kuliweka taifa kwenye taharuki.

"Taarifa hiyo ni ya uchochezi inayolenga kuliweka Taifa kwenye taharuki.  Mhe. Makamu wa Rais yuko bega kwa bega na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kufanya kazi zao kwa mujibu wa Katiba ya nchi ili kuwaletea wananchi maendeleo", imesema sehemu ya Taarifa hiyo na kuongeza;-

"Ofisi ya Makamu wa Rais inawataka wananchi na Watanzania kwa ujumla kupuuza taarifa hiyo ambayo inalenga kupotosha umma kuhusu ushirikiano mzuri uliopo baina ya Viongozi wetu". 
TAARIFA  RASMI

0 comments:

Post a Comment

Mdau, Uwanja huu ni wako, Toa maoni yako yasaidie kujua wewe unafikiri nini kifanyike kuboresha zaidi maisha ya Watanzania. Maoni yako yasilenge kuchochea mtafaruku katika jamii, kisiasa, kidini, kikabila au kijinsia. Mawasiliano yetu:- simu +255 (0) 712 498008, Email: nkoromo@gmail.com.
Bashir Nkoromo
Msimamizi Mkuu, Blog ya Taifa ya CCM.