Friday, September 9, 2016

KUTOKA BUNGENI:WAZIRI MKUU MHESHIMIWA KASIM MAJALIWA ASEMA SERIKALI HAIJALALA

WAZIRI MKUU MHESHIMIWA KASSIM MAJALIWA

Na Nassir Bakari.

WAZIRI MKUU wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa  Kassim Majaliwa amesema Serikali ya Awamu ya Tano haijalala na haijashindwa kuongoza nchi bali inafanya vitu vyake kwa weredi mkubwa.

"Serikali haijashindwa kuongoza nchi. Nataka niwahakikishie waheshimiwa Wabunge na wananchi wote kwamba tutaongoza nchi hii kwa mafanikio makubwa na kazi hiyo imeanza kwa marekebisho makubwa kwa maeneo ambayo tunadhani yatafanya Taifa hili liweze kupata mafanikio makubwa,” amesema.

Ametoa kauli hiyo jana, Bungeni mjini Dodoma wakati akijibu swali lililoulizwa na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni na Mbunge wa Hai, Bw. Freeman Mbowe, ambaye alitaka kufahamu Serikali ina mkakati gani wa kunusuru mdororo wa uchumi uliopo nchini.
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.