KINANA, PINDI CHANA WAKUTANA NA UJUMBE WA VIONGOZI WA NGAZI YA JUU WA CHAMA CHA MPLA CHA ANGOLA

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi, Ndugu, Abdulrahman Kinana (wanne kushoto), na Katibu wa Halmashauri Kuu, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Ndugu Pindi Chana (wa sita kushoto) wamekutana na Ujumbe ambao ni viongozi wa ngazi ya juu kutoka Chama cha MPLA cha Angola, kujadili namna bora ya kuimarisha uhusiano wa CCM na Chama hicho, na kufungua ushirikiano baina ya makada wake kwa fursa za mafunzo na itikadi.

MPLA na CCM ni miongoni mwa vyama sita (6) vya nchi za kusini mwa Afrika ambavyo vilishirikiana katika kupambana kuutokomeza ukoloni na vimeendelea kushirikiana kama vyama rafiki (sisters party).

Vyama hivyo chini ya uongozi wa CCM vinatarajia kujenga chuo kikuu kikubwa nchini Tanzania kwa ajili ya mafunzo kwa makada wa vyama hivyo juu ya itikadi, uenezi, ujasiriamali na uongozi.

Pichani Ndugu Kinana na Pindi Chana wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mazungumzo na ujumbe huo mjini Arusha, juzi.

0 comments:

Post a Comment

Mdau, Uwanja huu ni wako, Toa maoni yako yasaidie kujua wewe unafikiri nini kifanyike kuboresha zaidi maisha ya Watanzania. Maoni yako yasilenge kuchochea mtafaruku katika jamii, kisiasa, kidini, kikabila au kijinsia. Mawasiliano yetu:- simu +255 (0) 712 498008, Email: nkoromo@gmail.com.
Bashir Nkoromo
Msimamizi Mkuu, Blog ya Taifa ya CCM.