KENYATTA:HAKUNA MVUTANO KATI YA KENYA NA TANZANIA

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta (kulia) na akiteta jambo na rais wa Tanzania John Pombe Magufuli
 Na Nassir Bakari

 Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya, akizungumza mjini Mombasa wakati wa ufunguzi wa gati la makontena katika bandari ya Mombasa,   alikanusha ripoti za vyombo vya habari kwamba kuna mvutano baina ya Kenya na Tanzania.

“Vyombo vya habari vinaripoti kuwa kuna mgogoro baina yetu, lakini nataka kusema wazi wazi kwamba Kenya na Tanzania hazina mgogoro wowote baina yao,” alisema Kenyata.
Kenyatta alisema uchumi wa nchi hizo mbili umefungana kwa miaka mingi na ni kwa ajili ya faida ya watu wa nchi hizo mbili.


“Afrika Mashariki inashindana na dunia. Tunataka kujaliana (pale penye mapungufu). Tunataka tutumie nguvu zetu ili kukua, kuendeleza na kuinua uchumi wetu,” alisema.


Uvumi huo unaoripotiwa na vyombo vya habari unatokana na kutokuwepo kwa Rais John Magufuli  katika mkutano wa hivi karibuni wa kimataifa na Tokyo mjini uliofanyika mjini Nairobi, Kenya.


Mawasiliano ya aliyeandika story hii ni 0713 311 300

0 comments:

Post a Comment

Mdau, Uwanja huu ni wako, Toa maoni yako yasaidie kujua wewe unafikiri nini kifanyike kuboresha zaidi maisha ya Watanzania. Maoni yako yasilenge kuchochea mtafaruku katika jamii, kisiasa, kidini, kikabila au kijinsia. Mawasiliano yetu:- simu +255 (0) 712 498008, Email: nkoromo@gmail.com.
Bashir Nkoromo
Msimamizi Mkuu, Blog ya Taifa ya CCM.