LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 22, 2016

WAZIRI NAPE AKABIDHIWA LEO UWANJA WA UHURU BAADA YA KUKAMILIKA MATENGENEZO MAKUBWA

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, 
Naoe  Nnauye Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, 
Prof, Elisante Ole Gabriel, akibadilishana
 hati na Meneja wa Kampini ya CBG, Cheng Longhai,

 wakati wa makabidhiano serikali ikikabidhiwa 
Uwanja wa Uhuru, leo
Waziri wa Habari, Utamadhini Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amevitaka vyama vya Michezo nchini kujega Ofisi katika Uwanja wa Uhuru kwa kuwa mpaka sasa michoro kwa ajili ya majengo ndani ya Uwanja huo ipo tayari

“Kama kuna vyama vya michezo vyenye uwezo binafsi au kama wanaweza kupata ufadhili wa kuja kujenga ofisi zao humu michoro ipo tayari na eneo lipo tayari ata kesho waje wajenge ” alisema Mhe. Nape.

Mhe. Nape amesisitiza kuwa zoezi hili litaratibiwa na Serikali moja kwa moja na kutoa nafasi kwa vyama vyenye uwezo kujitokeza na kuchangamkia fursa hiyo ambapo  ramani,michoro na eneo lipo tayari kwa ajili ya zoezi hilo.

Aidha Serikali imewaalika wadau mbalimbali kuwekeza katika michezo kwa kujenga miundombinu itakayosaidia kukuza vipaji kwa wanamichezo mbalimbali na kusukuma gurudumu la  maendeleo ya sekta ya michezo nchini.

Kwa upande wake katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel amevishauri vyama vya michezo nchini kuchangamkia fursa iliyotolewa na Serikali ya kujenga ofisi za vyama vyao ndani ya Uwanja wa Uhuru na kushauri wadau wa michezo kuwekeza zaidi katika michezo hasa kwa vijana.


“ Wadau kimbilieni fursa ndio hii ya kuwekeza katika michezo pamoja na vyama vya michezo kujenga ofisi zao ndani ya Uwanja wa Uhuru kwa ajili ya maendeleo yao na michezo nchini” alisema Prof Gabriel.
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akiongozana na baadhi ya viongozi wa Wizara na Uwanja wa Uhuru mara baada ya kuwasili katika makabidhiano ya Uwanja wa Uhuru leo 22 Agosti 2016. KWA PICHA ZAIDI>>BOFYA HAPA

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages