LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 30, 2016

VITUO VYA REDIO MAGIC FM NA RADIO 5 VYAFUNGIWA KWA MDA USIOJULIKANA NA WAZIRI WA HABARI MHESHIMIWA NAPE NNAUYE KWA KUTOA TAARIFA ZA UCHOCHEZI






Na Nassir Bakari 0713 311 300

WAZIRI wa Habari, Utamaduni , Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye amezifungia Radio Magic Fm ya Dar es Salaam na Radio 5 iliyopo jijini Arusha kwa muda usiojulikana kutokana na madai ya uchochezi unaofanywa kwa makusudi kabisa na watangazaji wa Radio hizo.


Akizungumza na waandishi wa habari jana , Waziri Nape amesema kuwa uamuzi wa kuvifungia vituo hivyo umefikiwa baada ya kujirdhisha kuwa kipindi cha Matukio kilichorushwa Agosti 25, 2016 muda wa saa 2 usiku hadi saa 3 na kituo cha utangazji cha Radio 5 pamoja na kipindi cha Morning Magic katika kipengele cha Kupaka Rangi Agosti 17 vilikuwa na maudhui ya uchochezi unaoweza kuleta uvunjifu wa Amani.



Nape amesema kuwa kufuatia hilo amevifungia kwa muda usiojulikana kwani wamekiuka masharti ya kanuni ya 5 (a, b, c na d) , kanuni ya 6 (2a, b na c) na kanuni ya 218 ya huduma za utangazaji ya mwaka 2005.



Wakati vituo hivyo vikifungiwa kwa muda usiojulikana kamati ya maudhui imepewa jukuu la kuviita na kusikiliza kwa kina Zaidi utetezi wao na ni hatua gani zaidi ya kuchukua dhidi yao kwa mujibu wa kanuni ya huduma za utangazaji.


Mheshimiwa Nape ameendelea kuvitahadhalisha vyombo mbalimbali vya habari kutoa taarifa ambazo zina nia ya kudumisha amani na upendo uliopo kati ya watanzania na sio kuleta uchochezi.


No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages