Sunday, August 14, 2016

SPIKA WA BUNGE JOB NDUGAI "AFUNGUKA" KUHUSU MVUTANO WA WABUNGE WA UPINZANI NA NAIBU SPIKA

Spika wa Bunge Jog Ndugai
SPIKA wa Bunge, Job Ndugai asema bunge la Septemba atawaomba wabunge kujadiliana ili kuona wapi wanakosea ili “songombingo” iliyotokea bungeni iweze kumalizika.

Alisema anasikitishwa na bunge la sasa ambalo si moja limekuwa vipande vipande na kuelezea hali hiyo si dalili nzuri.

Spika Ndugai aliyasema hayo kwenye kipindi cha asubuhi cha Funguka, kinachopeperushwa na runinga ya Azam TV na kuongozwa na mtangaazaji Tido Mhando asubuhi Agosti 14, 2016.

Spika Ndugai ambaye wakati wa kikao cha bunge la bajeti kilichomalizika Julai, alikuwa nchini India akipatiwa matibabu, alisema kwa kawaida Wabunge wana njia mbalimbali za kuwasilisha malalamiko yao kama wanaona Spika, Naibu Spika au Mwenyekiti wa bunge hawatendei haki.

“Kutoka nje ya bunge, si kosa ni haki ya kidemokrasia, lakini zipo njia mbalimbali za kufikisha ujumbe kwa mujibu wa kanuni zetu,” alibainisha.

Spika Ndugai alisema, zipo hisia za kuonewa  kwa wabunge wa upinzani,

“Mbunge wa Upinzani anakatisha ruti (njia), ngumu kuliko mbunge wa CCM huko mtaani katika kugombea, kukumbana na polisi na kupita sero, sasa anapofika pale bungeni subira inakuwa ndogo, na akiguswa kidogo kumbukumbu yake inakuwa vile vile kuwa alaa kumbe na huku ni wale wale.” Alisema.

Spika Ndugai aliendelea kusema, pamoja na hayo lakini pia adhabu zilitolewa karibu karibu kwa wabunge hao, sasa hatua hiyo pia iliwafanya wabunge wa upinzani waone kama wameonewa, alisema.

“Tofauti na mpirani ukifanya kosa unapigwa kadi nyekundu pale palena kutolewa uwanjani, sisi bungni hatufanyi hivyo tunampa nafasi mbunge kujieleza, kala ya kuchukuliwa hatua yoyote.

Mtangazaji Tido alimuuliza Spika Ndugai “Ni jambo lililotia shaka baada ya Wabunge kadhaa wa upinzani tena wale  wenye uwezo wa kutoa hoja nzito nzito, ndio wameadhibiwa na hili linaleta hali tofauti.”

Spika Ndugai alisema, ni kweli wabunge hao ni wale wenye uwezo mkubwa, lakini spika au naibu spika hawapaswi kulaumiwa kwa kukazia kanuni, ambazo zimetungwa na wabunge wenyewe, labda jambo la msingi hapa ni wabunge hao hao wakae tena na kubadilisha kanuni hizo.

Akizungumzia kuhusu maridhiano, kati ya Wabunge wa upinzani, Wabunge wa CCM, na naibu Spika, Spika Ndugai alisema, atajaribu kufanya juhudi za kila namna ili kutafuta muafaka kwa pande hizo na ni imani yake kama wataridhia mazunhumzo hayo basi ufumbuzi utapatikana kinachotakiwa ni utayari wao.
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.